Msaada: Prado vs Nissan Murano

Yaleyale

JF-Expert Member
Aug 21, 2011
1,793
2,399
Wasalaam wanabodi.
Nimejichanga na napenda kununua gari la juu kidogo maana huku ninakokaa gari langu la chini kila siku naacha bamba kwenye makorongo.
Sina uzoefu na hizi gari, Prado ya 1998 na Murrano ya 2004 ndo chagua ninalofikiria kuchukua. Naomba ushauri kuhusu spear, uimara na confortability.
Nawashukuru sana in advance.
 
Salaam Yaleyale Mimi ni muuzaji wa magari mzoefu.

Kwa taarifa fupi hio uliyoitoa hapo juu, nimepata picha kua unapoishi mpaka kuifikia rami ni njia mbovu, napia nimegundua unahitaji gari iliyokwenye chati na ambayo ni imara na comfortable bila kusahau mwenendo wake wa mafuta.

Kanuni ya kwanza kwenye Biashara ni kumuweka MUNGU MBELE hii inaondoa tamaa, ambapo muuzaji hua huru kumuacha mteja achague mwenyewe baada ya kueleza ukweli halisi wakile
anachohitaji

MURRANO :

Nissan murrano ni.gari nzuri, yakisasa na ndani ipo comfortable sana, muundo wake ni mzuri ndani hadi nje (interiors and exteriors) na ikiwa kwenyebrami inatulia na mwendo mwanana sana, inshort ni gari nzuri, sana lakini ni (luxury)

Means huwezi ipeleka barabara zote (offroad)

PRADO :

Hii ni gari nzuri mno, ijapokua uzuri wake ndani unaweza usiwe kama murrano (inategemea na mtazamo wako) lakini ni gari yenye ubora wa hali ya juu mno, inakwenda barabara zote engine yakeinanguvu, na ni rafiki wa ainazote za mazingira ya barabara na pia body yake ni ngumutofauti na murrano.

Kikubwa zaidi, availability na hata namna ya utengenezaji, prado haipo complicated sana engine yake kama hizi murrano.

So kwa ushauri wangu, prado inakufaa zaidi kwa mazingira ya barabara ya unapokaa na pia ni gari ya heshima kwa watu wa rika zote (vijana kwa wazee inafit)

Hivyo, kazi ni kwako

Ikiwa utapenda Mimi nikuuzie, kati ya prado ama murrano (Kulingana na choice yako ), karibu inbox tujadiliane naweza kukuletea kwa bei nzuri tutakayo kubaliana!

Karibu sana!
 
Aksante sana mkuu magari7.
Nakutembelea inbox soon. Aksante sana.
 
Chukua prado tena ukipata ile ya cc 2700 iko poa sana unajua prado ni gari ambayo imekaa sokoni muda mrefu na haijachuja kwa hiyo hata ukitaka kuuza ni faster ama kubadilishana na mtu.
 
Prado nzuri, lakini kama uimara zaidi kwangu mimi I bet for Nissan Murano. Hata hivyo, chaguo ni lako.
 
Kweli kabisa kwa jinsi ilivyo Prado inahimili barabara mbaya wakati murano inafaa kwenye barabara nzuri
 
Kumbe!!! Maana mimi napenda sana safari ndefu tena nikiwa nadrive.
Hizo gari zishapoteza wengi tu, bolljoint za mbele sio kabisa zinakatika hovyo tu, kwangu mimi siwezi kusafiri nikiwa naendesha prado. Hata hivyo, uamuzi ni wako
 
BigBro : Naomba umuweke wazi nakumtoa picha ya kwamba prado zote ziko hivyo. For almost five years kuna mtu anatumia Prado na hua ni mtu anae safiri mno, na ameshasafiri nayo mpaka sasa zaidi ya mikoa nane ya tanzania

Mbeya
Musoma
Mwanza
Bukoba
Arusha
Kigoma
Sumbawanga
Tanga

Na kazi yake yeye ni geologist, anapokua anakwenda ni sehemu za mapori (vijijini ndani ndani kabisa)kwa muda wote huo hajawahi kukutana na hilo tatizo.

Sasa sidhani kama Murrano unaweza kuniambia inaweza kwenda kwa miaka yote hio safari ndefu kama hizo tena unaingia nayo off road , kama itaweza kuhimili mpaka sasa., let's be honest!
 
Mkuu sina tatizo la Prado, ila mimi binafsi naona Murano ni nzuri zaidi.
 
Hizo gari zishapoteza wengi tu, bolljoint za mbele sio kabisa zinakatika hovyo tu, kwangu mimi siwezi kusafiri nikiwa naendesha prado. Hata hivyo, uamuzi ni wako
Hii ni kwa prado zote? Am interested in
Third generation prado (J120: 2002–2009)
 
Prado ni gari nzuri hasa ground clearance ila shida ambayo nimeona last week nikiwa na gari ya rafik tukisafir musoma mugumu(rough road) haina balance hutakiwi kwepa mashimo ghafla hasa ukiwa spidi inayumba sana usipokuwa makini inakupiga chini...ila fuel consumption ni nzuri na inakimbia sana hasa rough road ndo raha zaidi achana na kitu land cruiser mjapan hakukosea ni kwa ajil ya barabara zetu..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom