msaada plz nimechoka kukaa kwa ndugu

Dada naona unataka uhuru wako vumilia umalize chuo upate uhuru wa kweli uondoke kwa mjomba ako ukiwa umeacha furaha na heshima itakusaidia katika maisha
 
Unachosema ni kweli kabisa tatizo watoto wa siku hizi hawana uvumilivu. Hakuna mama atakaekuchukia kama unatimiza wajibu wako. Inawezekana kukawa na tatizo upande wa shangazi lkn huna budi kunyenyekea tu . Nimeishi na mabinti wengi nyumbani kwangu yaani ni shida tu wanataka hadi dada awahudumie. Walikua radhi wakitoka shule wanaingia vyumbani mwao wanalala na kujifanya wanasoma. Kiukweli sitaki tena kuishi na ndugu mwisho wa siku wana lawama nyingi halafu mbaya zaidi hata wazazi wakati mwingine huwa hawatumii hekima huungana na watoto wao kukuumiza kinafsi. Hebu ona kama huyu anamwambia mjomba hapa nyumbani pamenishinda, hii si lugha nzuri.
 


uzuri na yeye ni mtt wa kike ataolewa na watakuja ndugu kama yeye alivyoenda kwa mjomba....atajionea mwenyewe jinsi alivyokuwa kero/mzigo kwa shangazi yake ndio ataona ni jinsi gani shangazi yake alimvumilia...

waliosema ndugu lawama hawajakosea kabisa,..kuishi na ndugu halafu aje kukushukuru ni wachache sana wengi wao wanaishia kulalama tu, hawana jema...hata mimi wamenichosha kwa kweli ni bora kuwasaidia huko huko waliko kuliko kuwaleta home manake mwisho wa siku wanageuka mwiba kwenye ndoa yenu na mahusiano yenu na ndugu wengine yanakuwa sio mazuri kutokana na maneno maneno..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…