Hapa karibu na ninapoishi kuna mama ntilie ana mdogo wake ambaye huwa anasaidiana nae kazi za hapa na pale,mimi nimekuwa na mazoea ya kwenda kupata msosi pale kwenye mgahawa wao pindi ninapokuwa sijaenda kazini. Yule binti alianza kunionyesha dalili za kunipenda ila mimi nikawa nampotezea maana nilikuwa bado na maumivu ya kuachwa na mpenzi wangu niliyedumu nae miaka mi4. Kila nilipokuwa naenda kupata msosi alikuwa akiongea maneno ya mafumbo ambayo yalinilenga mimi. Baada ya kwenda mara kwa mara nikajikuta na mimi nimeanza kumpenda,kila napotafuta mda wa kubonga nae nashindwa maana huwa anajichanganya na watu wengi,nikimuambia nina mazungumzo maalum na yeye huwa hanijibu chochote anakaa kimya kama hanisikii,je niendelee kumtongoza au nimpotezee pia nijitahidi nisimuone kabisa maana naona kama napoteza muda kwake