Msaada; photocopier Canon IR 2420

GX110

New Member
Oct 21, 2012
3
0
Natafuta copier hiyo brand new kwa bei nzuri ya sisi walalahoi tuliojiajiri. Nitapata wapi hapa dsm? Msaada tafadhali
 
Aah mbona zimejazana madukani mkuu?! Angalia kwenye vitabu vya TTCL yellow pages tafuta Ideal Computers Ltd utaona wako mtaa gani kwa hapo Dar kwa MZA wako Posta road karibu na Kuleana Restaurant. Pia kwa Mza utaipata The net kwa Tsh. 2.3m
 
cheki maduka near Masumi (kisutu) utapata zipo nyingi sana tena naona kama hazina wateja
 
nimetoka kununua hiyo ''canon ir 2420'' kama miezi2 iliyopita....
BRAND NEW inauzwa mil2 na laki moja masumin printways... Ila nlibishana nao wakapunguza elfu50.....
**kuna duka jingine kwa mbele linaitwa ZAMZAM nao wanauza brand new....
....direction .ukiwa kituo cha police mnazi mmoja upande wa pili wa barabara utaona nbc shuka na hiyo barabara kwa mbali utaona ghorofa/hotel... Karibia na hilo jengo upande wa kulia wa barabara wapo masumin na kwa mbele kuna zamzam
 
Natafuta copier hiyo brand new kwa bei nzuri ya sisi walalahoi tuliojiajiri. Nitapata wapi hapa dsm? Msaada tafadhali

Zipo nyingi tu, nimenunua last month! Masumin ni ghali sana, Nenda kwa Mod Tech mitaa hiyo hiyo ya kisutu au kariakoo Msimbazi opposite na jengo la club ya simba, nilinunua kwa Mod tech kwa Tshs.1.95, piga hii kuuliza 0222134899
 
Aah mbona zimejazana madukani mkuu?! Angalia kwenye vitabu vya TTCL yellow pages tafuta Ideal Computers Ltd utaona wako mtaa gani kwa hapo Dar kwa MZA wako Posta road karibu na Kuleana Restaurant. Pia kwa Mza utaipata The net kwa Tsh. 2.3m

Jamani namimi nimekuwa natafuta nikaambiwa aina hiyo aliyoitaja mwenzangu ndiyo nzuri
Jamani mbona ghali sana? Je haitapatikana medium size ambayo na bei inaweza kuwa nusu ya hiyo bei?
Nisaidieni na mimi jamani sina hela 2. million wapendwa biashara yangu bado ndogo sana
Nijibuni siwezi pata MEDIUM SIZE?
 
tafuta za mtumba/used... Ni nafuu ila ndiyo hivyo tena hujui historia yake ya ugonjwa....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom