msaada:njia za kujifunza programming kwa beginners

Aurelio_CSM

Member
Oct 14, 2014
57
22
Habarini za jioni wana jukwaa,
Nimemaliza kidato cha NNE nikiwa competent katika HTML na CSS na tayari nimefanikiwa kuanzisha project zangu 2 za website. Nimeanza kujifunza java Siku chache zilizopita kwa kutumia application ya solo learn. Ninataka nisome java pamoja android apps development ili niweze kutengeneza app kwa ajili ya hizi project zangu mbili. Tatizo ninakumbana nalo ni kuwa toka nimeanza kusoma nipo shallow sana kiasi kwamba nakumbuka syntax chache sana. Naombeni ushauri wenu nitumie njia zipi kusoma languages zote ninazotaka kwa urahisi huku nikipata mazoezi ambayo yatasaidia hizi code ziweze kustick kichwani. Ninatumia sana internet na pia sio mpenzi sana wa videos naomba kuelekezwa njia yoyote itakayonisaidia kujifunza huku nikipractice ninachojifunza mud a huo. Nia Yangu ni kukamilisha hizo project zangu mbili pia ninataman angalau nitakapoingia college niwe intermediate kidogo wa hizo languages ili niweze kusolve realllife problems kwa ujuzi Huu. Asanteni sana
 
Plz apply computer science au IT kuna mengi ya kujifunza kabla ya kuangalia hizo video za youtube fata hii njia nayokwambia ufanye mitihani ujue uwezo wako ndo uende youtube kuongeza maarifa
 
Habarini za jioni wana jukwaa,
Nimemaliza kidato cha NNE nikiwa competent katika HTML na CSS na tayari nimefanikiwa kuanzisha project zangu 2 za website. Nimeanza kujifunza java Siku chache zilizopita kwa kutumia application ya solo learn. Ninataka nisome java pamoja android apps development ili niweze kutengeneza app kwa ajili ya hizi project zangu mbili. Tatizo ninakumbana nalo ni kuwa toka nimeanza kusoma nipo shallow sana kiasi kwamba nakumbuka syntax chache sana. Naombeni ushauri wenu nitumie njia zipi kusoma languages zote ninazotaka kwa urahisi huku nikipata mazoezi ambayo yatasaidia hizi code ziweze kustick kichwani. Ninatumia sana internet na pia sio mpenzi sana wa videos naomba kuelekezwa njia yoyote itakayonisaidia kujifunza huku nikipractice ninachojifunza mud a huo. Nia Yangu ni kukamilisha hizo project zangu mbili pia ninataman angalau nitakapoingia college niwe intermediate kidogo wa hizo languages ili niweze kusolve realllife problems kwa ujuzi Huu. Asanteni sana
Syntax zinakuchanganya kwasababu umekalili nenda chuo dogo uelewe
 
Kama ni beginner, tafuta video za Lynda. Com zipo za almost language zote, kuanzia biginner, intermediate na advanced
 
Usipoteze muda kukariri syntax, ni wastage of time, wewe muda mwingi tumia kujifunza core language na how to program, syntax ni kitu ambacho kitakuja automatically kwa sababu utakua unarudiarudia mara kwa mara, ukikwama you can always go back and search for the syntax, hadi itakaa tu kichwani, so usiimbe syntax ka ngonjera.

Kuhusu kusoma watu tunatofautiana, wengine ni wagumu kuelewa hadi kuelekezwa so video zinasaidia, wengine wanadive into the books moja kwa moja na wanajikuta wanaelewa, swala ni kutafuta what works for you na kustick nacho.
Mazoezi unayotafuta wewe sijui ni yapi hasa, ila kama umesema unasoma Java kwa ajili ya android application, kwa nini usitengeneze app kama zoezi lako la kwanza?

Mfano, umemaliza kusoma how to create a layout, activities, fragments, unajua kudeal na listeners, how interfaces na abstract classes work, unaweza jipima kwa kujaribu kutengeneza app kama ya kutunza contacts, mtu anaregister new contacts inatunza kwenye sqlite database na kuretreave hizo data baadaye, unaweza include na picha pia, email e.t.c. Na kuifanya even more complex unaweza ongeza data kama kupima calls mtu alizopiga kwa namba flani.
Kitu kama hiki unaweza ukahisi hujui lakini the moment ukianza, ukishindwa unagoogle majibu yanakuja fasta, read code, write code, utajikuta umefika mbali sana. Kusoma tu all the time bila kutengeneza kitu chako mwenyewe nadhani ndio sababu upo hadi leo unalalamika syntax hazikai kichwani.
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom