chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 20,406
- 24,991
Habari ya siku ya Jumapili wanaJF.
Aidha nitangulize shukrani zangu kwa muumba wa vyote vilivyo hai na visivyo kwa ajili ya siku njema tena ya leo.
Nilete kwenu ombi langu la namna nzuri ya kuwadhibiti hawa mbwa koko ambao wafugaji wameshindwa kuwadhibiti na hatimaye wanatuletea usumbufu usio na sababu sisi majirani.
Mtu anafuga mbwa hampi chanjo ya kichaa cha mbwa, matokeo ni kuja kung'ata wapita njia wasiokuwa na hatia na kuwaachia ugonjwa hatimaye kufariki kizembe, mtu anafuga mbwa hamlishi chakula matokeo yake mbwa anarandaranda mitaani kula vinyesi na kila aina ya takataka na kuja kula mifugo ya watu mfano kuku n.k
Kiukweli nimeshaingizwa kwenye hasara kubwa na hawa mbwa koko kwani walishaingia kwenye banda langu la kuku na kuniachia manyoya tu. Ukimueleza jirani kuhusu mbwa wake kukutia hasara hakuelewi anakuwa na kiburi.Nimeshajaribu njia kadhaa hazijazaa matunda kwani kama siyo kuwatia kilema nimedhamiria kuwatoa uhai kabisa maana nimevumilia to the maximum.
Nimewahi kuwachanganyia sumu ya panya kwenye samaki lakini sikuwaona kama siku mbili hivi baadae walirudi tena kwa kasi kubwa, nadhani waliwahi maji ama vinginevyo. Sasa wakuu naomba tusaidiane MBINU hapa za kuwatokomeza kabisa hawa mbwa koko wanaotutia hasara na pia kutuweka hatarini kuambukizwa kichaa.
Nisingetaka kufika mbali sana kwenye ngazi za kipolisi ili kuripoti hili kama ipo njia rahisi ya kufanikisha.
Natanguliza shukrani.