Pvc zinafanya kazi vizuri tu. Frame unaweka za alminium.Naomba nichomekee kidogo kwenye uzi wako mkuu
Hivi ni kwa nini hawa watengenezaji wa plastic kama (kiboko,Jambo,Cello.etc)hawaoni fursa kama hii au kutengeneza milango ya plastic ambayo ingefaa kukaa chooni ama sehemu zenye majimaji!?
Kuna Technology ya PVC unaweza tengeneza Milango na madirisha, ipo nchini siku nyingi!Naomba nichomekee kidogo kwenye uzi wako mkuu
Hivi ni kwa nini hawa watengenezaji wa plastic kama (kiboko,Jambo,Cello.etc)hawaoni fursa kama hii au kutengeneza milango ya plastic ambayo ingefaa kukaa chooni ama sehemu zenye majimaji!?
Mkuu jiongeze. Inaweza kuwa nyumba ya kupanga. Vyoo ni vya kushare. Ila jamaa anataka ajijengee chake. Wewe cha msingi jibu swali usitake kudadisi mengineyo.Kwanini ni marufuku kujenga permanent?
Na kama ni hivyo kwanini uendelee kujenga hapo?
Safi, changamoto mbao zikipata maji huoza. Nilijua inawezekana kutumia mbao ila aluminium ilikuwa ni bora zaidi. Labda kwa kuwa ni ghali.Asanteni sana kwa mliochangia uzi kwa kunipa ushauri.
Nimeufanyia kazi ushauri wenu na kazi ilikuwa rahisi sana. Nilichukua mbao asubuhi na kutengeneza kibanda mraba cha 4ftx4ft (kama vile vya mawakala wa pesa) na kuacha 3ft sehemu ya mlango.
Kisha nikapachika pvc kwenye kuta zote jioni hii kwakuzivalisha kwenye zile lock zake kusha nikazifunga kwa screw. Kimekuwa kizuri sana utadhani ni tiles na ukimwaga maji yanateleza tuu. Kesho napumzika, keshokutwa nakamilisha kazi.