Msaada: Nini nifanye kwa huyu mzazi mwenzangu?

del moe

JF-Expert Member
Apr 4, 2016
827
1,023
Wasalam wana JF wenzangu

Ni binti niliekutana naye nakuanzisha mahusiano ambayo mwisho wa siku tukapata mtoto wa kiume. Katika kipindi cha uchauzito alipata mshikaji nakuishi nae Kama mke na mme.baada ya mtoto kuzaliwa nilijulishwa na mahitaji ya mtoto nikawa natoa Kama kawaida.

Baada ya muda vitibwi vikaanza ndani ya nyumba, bwana akaacha kutoa matumizi hata chakula ndani kikawa shida. Siku moja mtoto aliugua Sana akanipigia simu huku analia akidai mtoto Hari yake ni mbaya sana na hana pesa ya kumpeleka hospital. Nilimtumia pesa ambayo yote ma maelezo yake ilishia kwenye matibabu na kununua dawa. Ananiomba pia pesa ya matumizi. Nikwambia hayo Ni majukumu ya mume wake kwani mimi nahusika na mtoto wangu tu Basi.

Manyanyaso hayo yaliambana na kipigo hali iliyo pelekea arundi nyumbani kwao. Muda wote huo kwao hawanitambui kama Mimi ndiye baba wa mtoto na hajawahi kuwaambia imekuwa siri

Screen photo, niliweka picha niliyopiga Mimi na mtoto, kaka yake aliiona maana ni rafiki yangu sana ndio chanzo cha Mimi kufahamika kuwa ni baba wa mtoto. Vikao wakamwekea bi mdada matusi ya kutosha na kudai kuwa niende kujiripotisha,mmi nilikubali lakini nikamwambia walau nipatiwe mda nikusanye pesa maana siwezi kwenda ukweni mikono mitupu nikamwambia mwezi juni nitaenda.

Ugomvi uko hapa!
Wiki mbili zilizo pita nilimwomba nimwone mtoto akakubali na kumleta nilimpatia 10k.na kumwahidi baada ya siku tano nimpatia 30k.alikubari na kuondoka .

Ndani ya siku mbili alinipigia simu usiku na kuniuliza uko wapi nikwambia Niko nyumbani akakata simu.dakika shirini baadae kafika kwangu huku ana hasira hatari,nikamuliza nin shida... Ye Ni kufoka na kutukana akidai simjari Wala mtoto simchali. Nikamwambia Basi tulia Kwanza tuzungumze nikweleze nimekwama wapi na juhudi zangu Ni zipi. Hakutaka nisikiliza ikiwa funjo ndani naikona isewe tabu maana watu walianza jujaa. Nikampisha na kumwaja ndani

Siki iliyofuata asubuhi nikiwa najiandaa kwenda kwenye pilika zangu za Kila siku kaja tena akiwa na jazba zaidi ya Jana usiku nikamwomba tuzungumze kwa utaratibu lakini alikataa huku akitukana na kunitupia kadi ya bima ya afya ya mtoto (NHIF) huku akidai hataki kitu chochote kutoka kwangu na simu nisimtafute kuulizia Hari ya mtoto.

Baada ya siku tatu nilifaniwa kiasi cha 30k pesa niliyo mwahidi na kumtumia. Hakujibu kitu chochote Wala pesa hakurudisha.sasa nashindwa kumwelewa shida yake hasa , Kama mtoto me nahudumia.

Msaada ninaohitaji Ni:

1. Namna gani naweza pata haki ya kumwona na kumhudumia mtoto?

2. Kati ya Ustawi wa Jamii au Dawati la Jinsia ni wapi naweza saidika vizuri?

Naombeni msaada wenu wa mawazo maana mtoto ndio amefikisha miezi 16 sitaki akija kuwa mkubwa anichukie wakati uwezo wa kumpatia mahitaji yake ya msingi ninao.
 
Chakufanya, kawaeleze wazaz wake kila kitu mtoto wao anakufanyia...alaf ukae kimya, ipo siku atakutafuta tu.

Hata kwa MUNGU hutakuwa na hatia sababu moyo wa kutimiza wajibu wako unao kingine mtoto akiwa anaishi mazngra yasiyoridhisha tafadhali nenda ustawi wa jamii kadai mtoto ni haki yako ata kabla hajafkisha miaka 7.
 
Asante Sana nitafanya hivyo
Chakufanya, kawaeleze wazaz wake kila kitu mtoto wao anakufanyia...alaf ukae kimya, ipo siku atakutafuta tu,ata kwa MUNGU hutakuwa na hatia sababu moyo wa kutimiza wajibu wako unao. kingine mtoto akiwa anaishi mazngra yasiyoridhisha tafadhali nenda ustawi wa jamii kadai mtoto ni haki yako ata kabla hajafkisha miaka 7.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya mambo yako ya msingi na jiimarishe kiuchumi,uchumi ukiwa imara watakutafuta wenyewe.

Note: Baba tajiri hachukiwi hata siku moja na watakutafuta, ila baba masikini huchukiwa na hatafutwi.
 
Mzazi mwenzako ndio huyo kwa Dp?.

Anyway.
Kwasasa fanya unaloweza.
Fahamisha watu wachache wa familia yako. Fanya mishe zako kama kawaida.

Mambo mengine yatajiseti tu. Hakuna jinsi.

Kadi kaa nayo, mtoto akiumwa kama una hela tuma, kama huna peleka kadi.
 
Hahah unafanya kosa kubwa usiwe serious na hivi viumbe wewe kama baba na mwanaume endelea kufanya kazi na usitume chochote kuanzia sasa,kuwa na moyo wa kiume watakutafuta tu.

Huyo mwanamke bado mdogo hana akili ila mwanao akifika miaka mitatu tumia namna yoyote mchukue kwa lengo la kumsomesha maana huyo mwanamke atamwaribu mtoto baadae upate kazi nyingine kurekebisha mtoto
 
Back
Top Bottom