Msaada: Ninakwa na matone ya damu kipindi cha ujauzito

Msaada: Ninakwa na matone ya damu kipindi cha ujauzito

msakhara

JF-Expert Member
Joined
May 26, 2019
Posts
297
Reaction score
407
Habari wakuu... Kwa wale wataalamu wa afya au wazazi wenye uzoefu, naombeni ushauri wenu hapa "nina ujauzito wa miezi miwili, nimekutana na tone la damu kwenye nguo ya ndani mara mbili ndani ya week... Imenitia hofu sana!! "

Inaweza kuwa sababu ni nini?

Je, ninaweza vipi kuiepuka?
 
Wanasema light bleeding au spotting (matone) ni kawaida katika first trimester (miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito) ingawa hali hii haiwapati wanawake wote ni asilimia chache hupatwa nayo.

Wataalamu mtafafanua vizuri zaidi.
 
Oh! Please wahi nenda hospital sasa hivi. Onana na Gynaecologist. Kuna dawa utapewa. Sharti utakalopewa ni utulie ndani ukiwa umepumzika. Miezi 3 ya kwanza na miezi 3 ya mwisho inahitaji full bed rest.
 
Oh...kumbe Ni tatizo kubwa? Huwa linasababishwa na nini?
 
Sijui kwa kweli maana mimi si daktari. Nafahamu haya kwa uzoefu toka kwa mke wangu na rafiki zake. Ila nafikiri kipindi cha ujauzito kunakuwa na changamoto za homones na upungufu wa madini hasa madini ya chuma na zinc.
 
Mke wangu alipata hiyo dalili umri huohuo wa ujauzito.tulienda kwa Daktari wa uzazi,akapigwa ultra sound,akasema kiumbe hakionekani sababu umri bado mdogo.akatupa midawa flan hiv ghari sana,lakini baada ya mwezi kurudi kule na kumchukua vipimo tena tukaambiwa mimba imeshaharibika.

so story iliishia hapo,wala haikuwahi kutokea kipindi damu kutoka kwa wingi,ilikiwa ni vitone vitone,baadaye vikabadilika rangi,kama nyeusi,au damu ilipikwa.

So ushauri wangu wahi hospita mkuu
 
Wanasema light bleeding au spotting (matone) ni kawaida katika first trimester (miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito) ingawa hali hii haiwapati wanawake wote ni asilimia chache hupatwa nayo.

Wataalamu mtafafanua vizuri zaidi.
Literature zinasema hiv,hata mimi nilidharau baada ya kupitia literature za kwenye mtandao though she finaly miscaried

Ijapo alipata hiyo bed rest,nadhani ilikuwa tayari too late
 
Literature zinasema hiv,hata mimi nilidharau baada ya kupitia literature za kwenye mtandao though she finaly miscaried

Ijapo alipata hiyo bed rest,nadhani ilikuwa tayari too late
Pole mkuu. Ushauri wa muhimu ni kuwaona wataalamu wamshauri vizuri.
 
Mke wangu alipata hiyo dalili umri huohuo wa ujauzito.tulienda kwa Daktari wa uzazi,akapigwa ultra sound,akasema kiumbe hakionekani sababu umri bado mdogo.akatupa midawa flan hiv ghari sana,lakini baada ya mwezi kurudi kule na kumchukua vipimo tena tukaambiwa mimba imeshaharibika.
so story iliishia hapo,wala haikuwahi kutokea kipindi damu kutoka kwa wingi,ilikiwa ni vitone vitone,baadaye vikabadilika rangi,kama nyeusi,au damu ilipikwa.

So ushauri wangu wahi hospita mkuu
[emoji134][emoji134][emoji134]duuh... pole sana mkuu
 
Habari wakuu... Kwa wale wataalamu wa afya au wazazi wenye uzoefu, naombeni ushauri wenu hapa
"nina ujauzito wa miezi miwili, nimekutana na tone la damu kwenye nguo ya ndani mara mbili ndani ya week... Imenitia hofu sana!! "

Inaweza kuwa sababu ni nini?
Je ninaweza vipi kuiepuka?
DANGER!!
WAHI HOSPITALI HARAKA.
 
Habari wakuu... Kwa wale wataalamu wa afya au wazazi wenye uzoefu, naombeni ushauri wenu hapa "nina ujauzito wa miezi miwili, nimekutana na tone la damu kwenye nguo ya ndani mara mbili ndani ya week... Imenitia hofu sana!! "

Inaweza kuwa sababu ni nini?

Je, ninaweza vipi kuiepuka?
Habari
Si rahisi kupata jibu sahihi kwa tatizo halisi la mjamzito kwa maelezo tu kwani:

1: Matatizo haya huusisha kupata historia kamili ya hali ya kutoka damu pamoja na kuangaliwa mlango wa mji wa mimba kama umefunga au umefunguka pia pamoja na kufanya ultrasound.
Hii humpatia nafasi mhudumu wa afya kutoa jibu sahihi.

2: Wakati mwingine si rahisi kupaja jibu sahihi ya nini kimesababisha yaliyitokea kwenye namba moja hapo juu hasa kwenye miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Sana utaweza kuambiwa risk factors/visababishi vinavyofikiriwa kulingana na mgonjwa husika au kwa ujumla.

Ujumbe mhumu ni: fika hospitali na mwenza wako, usikilizwe na mhudumu wa afya, atafanya vipimo kwa kadri inavyofaa na kuwaeleza kama kuna shida au la. Nini kifanyike ili kuendelea kusonga mbele.
 
Kutoka kwa Damu ukeni kipindi cha Ujauzito yaweza kua moja kati ya dalili hatarishi katika kipindi hicho hivyo unapaswa kuhudhuria Clinic haraka iwezekanavyo pia zingatia mahudhurio yako ya Clinic bila kukosa kama tarehe zako zinavyoeleza.
Dalili hatarishi zinajumuisha na:
1.Kukosa nguvu
2.Kizunguzungu
3.Kutokuona vizuri/Ukungu
4.Kutokwa na maji maji yenye harufu kali ukeni n.k
 
ne
Habari wakuu... Kwa wale wataalamu wa afya au wazazi wenye uzoefu, naombeni ushauri wenu hapa "nina ujauzito wa miezi miwili, nimekutana na tone la damu kwenye nguo ya ndani mara mbili ndani ya week... Imenitia hofu sana!! "

Inaweza kuwa sababu ni nini?

Je, ninaweza vipi kuiepuka?
nenda hospitali
 
Back
Top Bottom