Msaada: Nina tatizo la kutoa majimaji puani

micind

JF-Expert Member
Jun 11, 2015
342
867
Habari zenu wanajukwaa,

Leo alfajiri nimeamka nikashangaa puani yanatoka majimaji Kama vile nosebleed lakini badala ya damu yametoka maji hayana harufu Wala hakuna maumivu puani lakini kichwa ndio kinauma Sana upande wa kushoto hiyo Hali imetokea Mara tatu ndani ya masaa sita,ikabidi niende hospitali nikapimwa full blood picture nikaonekana nina anaemia na pia daktari akasema inawezekana nina infection kichwani kwenye sehemu ya paji la uso (sinusitis) nikapewa dawa inaitwa cefpodoxime proxetil.

Tafadhali naomba msaada kwa aliyewahi kupata tatizo Kama langu alipata diagnosis gani kwa sababu hii Hali imenikosesha amani na pia daktari aliguess tu hiyo diagnosis baada ya vipimo vyote kuja negative na fbp kuonesha Nina anemia tu akaniambia nitumie hiyo dawa kwa siku tano Hali isipobadilika nirudi . Sasa wataalam naomba kujua mtu kutoa maji hivyo puani maana yake nini.

Asanteni.
 
Kapime sukari ,pia ni dalili za awali sukari ina dalili nyingi sana, hii nilisikia kwa shemejiangu akakutwa na sukari.
kama una kilo nyingi nakushauri jaribu kupunguza mwili na kula vyakula docta atakavyokushauri,

Ila njia bora yakupunguza mwili nikuepuka kula vyakula vizito hasa nyakati za usiku. Jitahidi sana kukaa muda mrefu bila kula ni tiba nzuri sana,
 
Sawa mkuu nitapima sukari though Sina uzito mkubwa Nina uzito wa kawaida kabisa hata leo hospitali nimeambiwa uzito wangu unaendana na urefu ingawa walinipima pressure kutokana na kuwaambia naumwa Sana kichwa hasa usiku.
 
Habari zenu wanajukwaa,

Leo alfajiri nimeamka nikashangaa puani yanatoka majimaji Kama vile nosebleed lakini badala ya damu yametoka maji hayana harufu Wala hakuna maumivu puani lakini kichwa ndio kinauma Sana upande wa kushoto hiyo Hali imetokea Mara tatu ndani ya masaa sita,ikabidi niende hospitali nikapimwa full blood picture nikaonekana nina anaemia na pia daktari akasema inawezekana nina infection kichwani kwenye sehemu ya paji la uso (sinusitis) nikapewa dawa inaitwa cefpodoxime proxetil.

Tafadhali naomba msaada kwa aliyewahi kupata tatizo Kama langu alipata diagnosis gani kwa sababu hii Hali imenikosesha amani na pia daktari aliguess tu hiyo diagnosis baada ya vipimo vyote kuja negative na fbp kuonesha Nina anemia tu akaniambia nitumie hiyo dawa kwa siku tano Hali isipobadilika nirudi . Sasa wataalam naomba kujua mtu kutoa maji hivyo puani maana yake nini.
Asanteni

Pole sana
Ngoja waje wataalamu
 
Back
Top Bottom