God'sBeliever
JF-Expert Member
- Sep 1, 2015
- 5,788
- 3,062
Kuna mda unafika najiona niko tofauti na binadamu wenzangu. Unaweza kuta tupo msibani, ajali au kwenye tukio la mauaji unakuta watu wote wako na huzuni ila mimi niko freshi na nina amani kabisa moyoni wala siwazi yani nachukulia ni jambo la kawaida tuu.
Hata wakati wa usiku wa manene huwa siogopi kutembea nje na hata kama hilo eneo lina mashetani au linahisiwa vibaya mimi napita tuu. Nina hasira za karibu sana na huwa nikigombana na mtu huwa sinaga time nae tena na hata tukija kupatana ni baada ya miaka mingi sana. Hali hii imenifanya kuwa mtu wa visasi na huwa sikubaligi kushindwa jambo kabisa, niko radhi nirudi nipambane na nishinde hilo jambo.
Huwaga najipenda mwenyewe kwanza halafu ndio naangalia na wengine. Ndugu zangu hata wakifa mimi naona poa tuu na ninavyowaandikia hapa baba yangu ni marehemu na bado halinipi shida mimi naona kitu kidogo tuu.
Hata wazazi wangu nawachukuliwa kawaida tuu hata siwaogopi. Shuleni nimewahi kuwa na uadui na wale wababe wa shule na kwanza nilikua sinaga time nao. Kuna mmoja aliwahi kuniambia nina dharau mimi sikumjibu nikaendelea na mambo yangu. Kuna mmoja alinipiga mgongoni hiyo ndo ikawa safari hadi saivi natamani nikamchome kisu.
Mimi raha yangu ni kusikia watu nisiowapenda wamepata matatizo hata kufa kabisa. Mimi watu ninaowapenda ni wale wauaji na makatili waliowahi kutokea hapa duniani. Mimi sipendagi kuonewa kabisa ila nikiona mtu anaonewa ambae hana hatia huwaga nakasirika sana na sa nyingine kuokoa huyo mtu.
Nimekua sina mda sana na wanawake, wakiniletea za kuleta nawapiga chini naendelea na maisha yangu peke yangu, msichana yeyote akinisma vibaya mimi namfata nampiga makofi naondoka zangu maana mimi si mtu wa maneno.
Nimekua na kiburi mno hata ndugu zangu wanalitambua hili na hii imefanya baadhi ya watu wengi kuniogopa sana.
Sasa wakuu kama nilivyojielezea hapo nawezaje kuepukana na hali yangu hii niliyonayo?
Nawasilisha.