Msaada: Nimetoa pesa kwenye ATM haikutoka ila salio la awali limepungua

hapo inategemea kama ww ni mteja wa bank ya NMB Au ni mteja wa bank nyingine lakini ulitumia ATM ya bank ya NMB kama ww ni mteja wa NMB it's easy to refund ela yako baada ya kupitia miamala ya cku hyo ktk ATM husika kama ela aikutoka lazima itakuwa imebaki ktk roller so ukienda ku clame watakurudishia fedha yako nadhani huwa ni baada ya cku 2-7

pia kama ww ni mteja wa bank nyingine ukatumia ATM ya NMB kwanza inatakiwa urudi kwenye branch ya bank yako andika barua kwa manager wa tawi la bank yako elezea situation ilivyo kuwa pia ktk maelezo yako usisahau kuandika tarehe, muda na cku lilipotokea ilo tatizo pia namba yako ya card ya ATM na account number ya iliyokuwa unataka kutoa hzo fedha then bank yako ndo watakuwa responsible kufatilia madai yako kwa NMB kama sheria na taratibu zinavyowataka swala hili uchukua cku14-45 kupata fedha yako
Ni mteja wa NMB
 
Ni tatizo la kawaida na huwa linawatokea wengi. Pesa yako itarudishwa usihofu kabisa. Ukipata wasaa nenda benk waeleze siku na muda na pesa uliyokuwa unatoa utarudishiwa pesa yako. Mara nyingi huwa wanarudisha wenyewe hata wewe usipokwenda.
Iwapo sijakwenda inaweza kurudishwa Hivyo Hivyo nimeangalia sasa Hivi naona bado haijarudishwa
 
Mkuu nenda Bank iliyopo karibu kuna form utapewa ujaze then wakifanya mlinganisho watakurudishia
 
Mm siku hizi kabla sijatoa hela naangalia salio kama ndilo nililoliacha kipindi cha mwisho.. Huchelewi kukuta salio limemegwa. Mkuu nenda bank na hizo risiti watakurejeshea salio lako. Bank za bongo ni shida sana.
CRDB kila siku jioni saa 12 hivi ATM zote zinakua hazifanyi kazi eti wanafunga mahesabu. Nonsense,hivi wanapoteza shilingi ngapi kufanya hivyo,hivi wanawajua wanawasumbua wateja wao kiasi gani.
Bado tuna asafari ndefu kufika nchi ya ahadi
 
Mimi niliwahi kutoa laki mbili kwenye ATM na wakati mashine ikihesabu umeme ukakatika. Kadi ilitoka lakini pesa haikotoka na nilijagundua kiasi kile cha pesa kilipunguzwa ktk account yangu na hadi leo sikurudishiwa
Mkuu kuna uwezekano mkubwa kua baada ya umeme kurudi Pesa zako zilitoka coz process ilikua imeshakamilika na ndio maana kadi yako ilitoka,Pole sana aisee.
 
Iwapo sijakwenda inaweza kurudishwa Hivyo Hivyo nimeangalia sasa Hivi naona bado haijarudishwa
Inarudishwa baada ya kufanya reconcilition ya miamala ambayo ATM ilifanya. Ila kama kadi yako ni ya benki tofauti na ATM uliyoenda kutoa pesa, ni lazima uende kwenye benki yako kuna fomu utajazishwa. Ila kama kadi yako na ATM ni ya benki hiyohiyo, hata usipokwenda utarudishiwa ndani ya siku muda mfupi ila ukiona unakosa amani unaweza kwenda tu hata j3 haina shida utahudumiwa kirahisi sana.
 
Wakuu nilienda NMB bank kutoa kiasi cha fedha mara ya kwanza ATM machine Ilikuwa inahesabu Lakin pesa haikutoka zaidi ya risiti na kadi pekee

kwenye risiti kunaonyesha Huduma haijakamilika Lakin kiasi kilichopo mwanzo kimepungua

Mara ya Pili haikuhesabu Lakin Pia pesa haikutoka na pesa imepungua tena risiti imeandikwa vilevile Huduma haijakamilika

Je naweza kurejeshewa kiasi kilichoonekana kimetoka Lakin sijafanikiwa kukipokea??au hadi niende kwenye tawi la bank husika
Nenda kwenye tawi lako watairudisha. Hela kama haijatoka inaonekana kwenye system usiwe na wasiwasi. Mimi imenitokea mara kadhaa na mara zote zilirejeshwa baada ya kwenda kutoa taarifa.
 
Mm siku hizi kabla sijatoa hela naangalia salio kama ndilo nililoliacha kipindi cha mwisho.. Huchelewi kukuta salio limemegwa. Mkuu nenda bank na hizo risiti watakurejeshea salio lako. Bank za bongo ni shida sana.
CRDB kila siku jioni saa 12 hivi ATM zote zinakua hazifanyi kazi eti wanafunga mahesabu. Nonsense,hivi wanapoteza shilingi ngapi kufanya hivyo,hivi wanawajua wanawasumbua wateja wao kiasi gani.
Bado tuna asafari ndefu kufika nchi ya ahadi
Yenye kujiri katika Africa yetu yataka uvumilivu
 
Inarudishwa baada ya kufanya reconcilition ya miamala ambayo ATM ilifanya. Ila kama kadi yako ni ya benki tofauti na ATM uliyoenda kutoa pesa, ni lazima uende kwenye benki yako kuna fomu utajazishwa. Ila kama kadi yako na ATM ni ya benki hiyohiyo, hata usipokwenda utarudishiwa ndani ya siku muda mfupi ila ukiona unakosa amani unaweza kwenda tu hata j3 haina shida utahudumiwa kirahisi sana.
Shukran Mkuu kwa mnyambulisho yakinifu ubarikiwe sana
 
Mkuu hiyo huwa inatokea sijui kwanini hawapo makini.Nakumbuka nilienda ATM moja hivi mida ya saa 4 usiku nilikuwa na dharura ile nafika pale nikakutana na mjeda ndo anatoka kutoa pesa akanambia system ipo down hajafanikiwa kutoa hela.Nikasema kwakuwa nina dharura ngoja nisubiri kidogo nami nijaribu.Muda kama dakika 5 hivi nashangaa mashine inatema hela mfululizo.Nikabaki nimeduwaa peke yangu mlinzi yupo maeneo ya benk anafanya patrol ya lindo.Zilitoka kiasi kikubwa sana nikajizolea mpunga wa kutosha huyooo sikuhangaika hata kuingia kadi yangu tena.Nafikiri watu wengi walioambiwa huduma haijakamilika ndo hela zao zilikuwa zinatoka mfululizo baada ya system kurudi.

Daaaaah kuna watu mna bahatiii
 
Technological failure inaweza kitokea popote. Hata ndege za mashirika makubwa huanguka due to technical failure. Tuache mentality ya kujidharau sana, hii tabia sio nzuri na imeanza kukua sana nchini ktk miaka ya hivi karibuni.
Wewe kakojoe ulale,hujui unaandika nini,nimezunguka dunia nzima mara 11 sijawahi kuona kitu kama hicho hata kusoma popote,unaejidharau ni wewe shwaiiiin ulioko kijijini kulinganisha ATM na AIR accident.
 
Mimi niliwahi kutoa laki mbili kwenye ATM na wakati mashine ikihesabu umeme ukakatika. Kadi ilitoka lakini pesa haikotoka na nilijagundua kiasi kile cha pesa kilipunguzwa ktk account yangu na hadi leo sikurudishiwa
Ulienda kuriport benki? Imewahi kunitokea exactly kama wewe ila nilienda kuripot nkajaza form maalum then ndani ya 24hrs ikarudi
 
Km imechanga maybe kuna tatzo kwenye dispenser ndani ya ATM lakini usijali wanaweza wakakurefund au nenda jtatu branch watakurefund kwa kujaza form
 
Mimi niliwahi kutoa laki mbili kwenye ATM na wakati mashine ikihesabu umeme ukakatika. Kadi ilitoka lakini pesa haikotoka na nilijagundua kiasi kile cha pesa kilipunguzwa ktk account yangu na hadi leo sikurudishiwa
Nenda branch husika ya bank watakupa form utajaza then pesa utapata, card kurudishwa wakat umeme umekata kuna back up battery imefungwa kwenye card reader so hata km umeme ukikata card reader inakuwa na power
 
Pole sn,nenda ofisini kwao j3 kuna form unajaza,ambatanisha kopy ya kitambulisho na risiti hiyo inayosema muamala umekamilika/haujakamilika thn utapewa 5 working days watakurefund pesa yako,hkn namna nyingine,pesa zako ziko salama,mimi imeshanitokea na hizo ndo process
 
Back
Top Bottom