Msaada: Nimetekwa China

Siwezi kabisa mkuu hiyo ni kazi ya MUNGU.
Na sio wawili tuu... nimesema hao wawili ni watanzania niliokuja nao kama wanafunzi.
Nyuma yao kuna kundi kubwa sana la watu.
Yote namuachia Mwenyezi-Mungu.
Kumbuka huwezi shindana na walimwengu.
 
Siwezi kabisa mkuu hiyo ni kazi ya MUNGU.
Na sio wawili tuu... nimesema hao wawili ni watanzania niliokuja nao kama wanafunzi.
Nyuma yao kuna kundi kubwa sana la watu.
Yote namuachia Mwenyezi-Mungu.
Kumbuka huwezi shindana na walimwengu.
kwahiyo unaamini kabisa mungu atawazuia kujutatua marinda
 
Mbona nchi hii kuna watu WA upinzani wengi Tu wanasomq na wanagraduate?? Iweje wewe Tu ndo ufuatiliwe mpaka China?? Una nn cha ziada hebu tuambie Mr. Kisandu
 
Mimi sijaelewa mara Mama yako mara CCM inawezekena kwenye nyaya zako kichwani kuna sehemu zimekata
 
Kwa mfano hata hapa utawaona wanavyokuja negatively kunikaisha tamaa eti nilichoandika hakieleweki though najua sijui kupangilia matukio vizuri ila
hapa mwenye nia njema ataelewa kitu... haters watakanusha na kutoa kejeli.

Ndugu ulichoandika sio tu kwamba hukupangilia vizuri ila pia ni kweli hueleweki, kwanza hujasema huko kuanzia RUCU mpaka Iringa university ulichofanyiwa, sasa unahitaji msaada halafu huwi wazi watu wakuelewe wajue wanakusaidiaje, pili habari ndefu tena kama yako isiyo wazi (maana angalau ingekuwa wazi inaweza kumvutia msomaji akafika mwisho hata kama ni ndefu) inachosha na nna uhakika kati ya waliosoma kisa chako wengi hawajamaliza, hivyo jitahidi kufupisha habari yako!!!
 
kama huwezi kushindana nao... jiunge nao
but kwa malengo yako then yakitimia 'utajua mwenyewe what to do...
 
Kweli wangekuwa wanakufatilia na kukubana ungepata muda wa Kuandika thread ndefu hii? Ucha ukichaa dogo
 
Mkuu, kwa maelezo yako ni ngumu kujua unahitaji msaada gani.

Umedai wanakutesa kwa 'vita ya kimwili isiyoonekana(kichawi)', upo kifungoni, upo na wanaCCM (watanzania) ambao unaishi nao chumba kimoja.Unaweza kusema kama wamekutesa au kukufanyia umafia wowote kimwili?

Hilo la kichawi unauhakika gani?

NB: Kama kuna mtanzania kwenye huo mji akamfate huyu bwana amsaidie, anahitajika hospitali.It's like haelewani na mtu yoyote kuanzia nyumbani kwao hadi chuoni.
 
Mkuu, ahsante kwa ushauri wako.

Ni dhahiri kwamba Joseph anahitaji kumwona daktari.Ila kwa tatizo lake unadhani atatuelewa kweli tunavyomwandikia hapa?Nadhani akili ishajiset kwamba yote haya ni hao jamaa wa CCM ndio wanasababisha.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…