Msaada: Nimetekwa China

Pole sana, nimefuatilia Uzi wako A-Z ila nimegundua ni uongo tu! Yaani wewe uliyemaliza Form 6_ 2015 Leo hii 2018 una lipi LA maana hadi ufuatiliwe na CCM kiasi hicho? Yaani CCM yaani wewe uliyemaliza form six 2015, leo CCM itumie hadi Freemasonry kukufuata wewe? Unasema mama yako anahusika hata kama lakini sidhani kama unahitajika kiasi hicho huko CCM. Hivi MTU kama FATUMA KARUME mtoto ambaye ametokea kwenye familia ya CCM na sasa hivi anaipinga sana sidhani kama anafuatiliwa hivi! Alafu unaongea kwa parables tu, kama ingekuwa ni kweli na unateseka kiivyo usingetumia Parables . Acha utoto ndugu
 
Mwanamapinduzi unashindwaje kupinduka mbele ya unaotaka wakupe mapinduzi....

We sio mwanaharakati teena... We ni mtekwaji... Unawaomba amnesty wakuokoe... It means ushafeli.


Ila kaza tu hakuna harakati bila maumivu....

Si umejitakia.. Km kweli we komaa tu... Iwe siri yako... Hata mandela alikaa jela... Sembuse wewe uko ghetto teena china teena unachat...

We kaza tu man... Binafsi sina msaada na hata ningekuwa nao nisingetoa kwa mambo ya kujitakia....
 
Mkuu kichwa ulichoanza nacho hakiendani kabisa na stori yako, yani umenishtua mpaka nikaanza kuandaa ransom nikijua umetekwa daah jifunze kuandika na kuopen up kama ni kweli mana fiction stories in jf are too much
 
 
Kwa aliyeelewa anihadithie.
Maana naona jamaa kama Dr. toka kule USSR ya zamani.
yani hata yule dr alijielezea vizuri akawa anaeleweka maana hapa tumechangaywa kweli keli....mara mapepo, kuna swala la elimu, kuna swala la nyota na matayo hapo hapo unaambiwa kama hujaelewa na we ni pepo kutoka chama tawala! khaaa
 

Mkuu wewe ni kiongozi mkubwa sana hapo kenye hicho chama ulichopo?
 
Pychosis at work. I smell Deo Kisandu here!! Usipowahi Milembe jiandae kuokota makopo!
 
Mmh I know you are not faking... But please take my advice....
 
Sikia nikuambie wewe nimesema nilianza kuhangaishwa chuoni huko mwaka 2016 hapo nilikua na miaka 21!
Siasa ningafanya wapi wakati ndio kwanza nilikua nasoma... na nikuambie tuu mimi nilikua sipendi siasa ili nilitamani siku moja CCM itolewe madarakani ndio maana wazee wakitengo walinisoma sasa wakaona gia ya kunipata ni kunipa mateso...

Vitu vingine kama hujui ni bora uulize ila kama umekuja kukana hapa its okay maana ndio kazi yenu... nawaona mnavyopinga kwa nguvu zote hapa ila niwaambie tuu mambo yenu yanafahamika everywhere hapa ni kama kutwanga maji kwenye kinu.

NB: Mtu wao wanaemtaka huwa wanamchimba toka utotoni kama ulikua hujui naomba utambue hilo! Ndio ukisikia watu wanaandaliwa ujue walishatazamwa toka utotoni. That's background check... unaowaona walioko juu usifikiri walijikuta wapo hapo juu tuu.
Kilichofanyika kwenye hivyo vyuo sio kigeni kwani ndipo vijana wanapotafutwa.
I hope nimekufungua kidogo au kama ni mamluki its okay simply because i expected you here kama kawaida yenu.
 
Wewe si mzima wa akili
 
Mkuu sijafanikiwa kuelewa japo kwa kiasi fulani nimevutiwa na simulizi lako kuna mambo mengi ningependa kujua kutoka kwako ila inaonekana sio mtu wa mchezo mchezo huko china unaishi kwa pesa ya nani kwanza tuanzie hapo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…