Msaada: Nimetapeliwa milioni 1

Majigo

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
5,519
1,826
Wiki 1 iliyopita, rafiki yangu kapatwa na maswahibu ya kusikitisha mno.!
Yeye ni muajiriwa katika duka la kutoa na kuweka pesa kwenye mitandao ya simu!Kuna jamaa akaja kuweka pesa tsh milion 2 baada ya kumtumia zile hela na kuondoka.Akabaini mil 1 kati ya zile hela, toka kwa yule jamaa ni feki (hakuwa mzoefu kujua uharali wa fedha).

Amechanganyikiwa kwani namba ya yule mwizi, haipatikani hadi sasa na hatujui la kufanya! Bosi amemkaba alipe hela zilizopotea.

Jana kanipa taarifa hii na ameomba ushauri atazipata vipi hela zake kwani kwa sasa ana mzigo wa kulipa deni, kupitia mshahara wake.

Karibuni wakuu..Pia Samahani kwa kuwachosha!

Jigo
 
Poleni sana, hapo hana anachoweza kufanya,hata kama namba ya huyo tapeli ukiipata haisaidii, maana kama hakuweza kutambua hizo noti feki wakati jamaa akiwa bado eneo la tukio hakuna tena ushahidi wa kumuhusisha huyo tapeli na hizo noti feki.Hii biashara inahitaji uangalifu wa hali ya juu sana.
 
ndio kashakimbia huyo akubal tu kukatwa deni na mwajir wake... next time awe muangallifu
 
Awapelekee polisi huwa wanajua jinsi ya kuzitumia.
Mtuhumiwa ukifika kituoni unasachiwa wanakusweka ndani kesho
yake unaachiwa kwa dhamana na kubambikizwa noti bandia na dhamana inafutwa
na balance yako ulioendanayo wanalamba.
jioni wanapiga viroba kama kawaida.
 
dah! Wakuu asanteni sana Lakini ingewezekana kumpata huyo mwizi ningeshukuru sana!

Jigo
 
Ukisha tapelewa umetapelwa tu,
Afadhali ya yeye katapeliwa kiduchi,
kuna watu wametapeliwa ooohhh
 
next tym mwambie boss wake abandike note fake hii ni njia ya kuwaonesha/kuwatisha na kuwa makini kuzifaninisha na zile but noti halal huwa zinakaharufu kake na huwa zinamng'ao wake ang'avu but noti fake lipolipo tu
 
Back
Top Bottom