Msaada: Nimesahau password ya simu yangu

mwanamimi

JF-Expert Member
Joined
Oct 30, 2017
Posts
265
Reaction score
181
Wakuu, nategemea mu wazima wa afya na mnaendelea na majukumu kama kawaida.

Wakuu simu yangu nilibadili password kwa bahati mbaya nilisahau password mpya niliyoiweka. Nimeshidwa kuifungua, naombeni msaada wa jinsi ya ku-unlock simu hiyo. Model ya simu in Wiko Lenny 4 plus.
 
Kabla ya kufanya chochote zima simu kwanza. Inazimika ubinye power botton hadi izmike,au kama unashindwa ubinye button ya power na v- hadi izime. Kama ni simu ya button mbele inatakiwa ubinye volume up+ power button simulteneously mpaka itokee either gear au android logo au maandishi madogo ya rangi ya blue.

Then utumie v+ kuselect mpaka ufike reset to factory setting, subiri mpaka iandike complete, then select tena clear cache halafu subiri tena, then chagua reboot, subiri mpaka iwake na ufanye tena setting ya simu.
 
Mkuu nimefika hapo ila nikiweka kwenye reboot ila inagoma.ngoja nijaribu sasa nitakuletea mrejesho.
 
Asante kwa ushauri wako. Ikishindikana hard resert nitaipeleka kwa fundi kesho
 
Basi fanya hard reset ila huwezi okoa chochote humo
Kuokoa matatizo kama hayo penda kusave vitu vyako muhimu kupitia Google Drive ina GB 15 za free unaweka humo kuondokana na stress kama hizi.
 
Kesho ataleta mrejesho ila lazima apoteze kitu ili simu ipone
 
Mkuu nisaidie hapa kwenye kuset email nimesahau nataka kuweka nyingine inawezekana?
Haiwezekani ingekuwa rahisi kama unajua hata email yako alafu password ndio umesahau hapo ni kuflash tu au ujanja mmoja vipi ni process kuifanya itoke hiyo email
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…