Msaada: NIDA yangu imefungiwa

Habari. Jana nilikuwa nataka kusajiri line mpya ila imenigomea naambiwa namba ya NIDA imezuiliwa naomba msaada kwa mwenye uzoefu nifanye ili nida yangu ifunguliwe. Na ni mitandao miwili tu niliyosajiria nida yangu VODA NA AIRTEL
Acha kuitumia kwa kuwasajilia wengine, huo ni uhalifu japo wewe unaona ni ujanja! Usije tena huku kutuomba ushauri ili uendeleze uhalifu.
 
Nimekwenda sehemu wanaposajiri line, nilitaka kusajiri line ya halotel mhusika baada ya kuanza process mhusika akaniambia namba yangu ya nida imefungiwa hivyo siwezi sajiri line mpya
Wewe ndo wale wa tuma kwa hii namba, polisi wangekuwa karibu wangekukamata.
 
Hivi karibuni TCRA kuna faini walitoza kampuni za mawasiliano, baadhi ya makosa ni kampuni kutumia kitambulisho kimoja kusajili zaidi ya idadi ya namba 5. Hii inaweza kuwa sababu ya tatizo halilopata huyu mdau.
 
Kama namba yako ya Nida imehusika kusajili line iliyohusika katika uhalifu wa aina yoyote polisi hufungia namba hiyo ya NIDA,so kumbuka vizuri kama hujawahi husika na maghumashi yoyote
 
Nenda ofisi za Vodacom watakufungulia.
NB: NIDA watakurudisha hukohuko Vodacom.
Shukran sana mkuu, hii imenisaidia, nimeenda ofisi za Vodacom wamewasiliana na NIDA kujua tatizo nini, then wameifungua now ipo fresh. Ubarikiwe sana
Nenda ofisi za Vodacom watakufungulia.
NB: NIDA watakurudisha hukohuko Vodacom.
 
Shukran sana mkuu, hii imenisaidia, nimeenda ofisi za Vodacom wamewasiliana na NIDA kujua tatizo nini, then wameifungua now ipo fresh. Ubarikiwe sana
Next time kua makini... Acha kusajili laini mtaani kwa hawa mawakala njaa wanaojifanya wanasajili laini bure kumbe kuna namna wanajilipa kwa udanganyifu! Ukitaka kuongeza laini fika SHOP ya mtandao husika kabisa ndo usajili..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…