Msaada: Ni nani msemaji wa serikali

E84

Member
Joined
Jul 27, 2016
Posts
6
Reaction score
5
Nimekua nikifuatilia shughuli nyingi za kkiserikali na kuona kila taasisi ina msemaji wake. Je pale linapokuja suala la kitaifa ambalo si la taasisi mahususi ni nani anayekuwa msemaji wake? Je ni waziri wa habari, katibu mkuu kiongozi au mkurugenzi wa habari maelezo?
 
Nchi hii hakuna msemaji wa serikali kwa sababu kila anayejiona ana wadhifa fulani ni kambale na sharubu zake!
 
Msemaji wa serikali anatakiwa awe na uwezo mkubwa wa uelewa wa mambo mengi ya kijamii, kiuchumi na kisiasa ndani na nje ya nchi pindi naposma jambo lolote inamaana anawasilisha taswira ya Nchi na Serikali...hapa kwetu najua msemaji wa ikulu ndiyo msemaji wa serikali kama sivyo naomba kusahihishwa.
 
Kukujibu.
Inategemea na eneo, ie kila eneo lina wizara yake.
Kama ni la kitaifa kutegemea na uzito wake basi ipo Ofisi ya PM au zito zaidi Ofisi ya Rais.
Na yote hupitia idara ya habari maelezo
 
Mfano wa suala, ni suala gani kwa mfano?
 
Kwenye serikali simjuwi nani hivyo kwa sasa nakubaliana na wewe hadi hapo nitakapopata uelewa mwingine kinyume na huu ila katika serikali ya JK msemaji wa mambo yote ya kitaifa na ambae alikua anaimudu nafasi hiyo alikua muhshimiwa membe
 
Mfano wa suala, ni suala gani kwa mfano?
Yako mengi kwa mfano:
Waislamu wa Tanzania wajiunge au wasijinge na oic au kuundwa ama kutokundwa kwa mahakama ya kazwi au uwepo au kutokuwepo kwa uraia wa nchi mbili wa mtanzania na mfano wa hayo
 
Oyaaa hili bwawa la kambale, kila mmoja ana ndevu so hainaga msemaji hiyo....[emoji16][emoji16]
 
Msemaji Mkuu wa serikal ni Zamaradi Kawawa.
Msemaji Mkuu wa Nchi ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo.
Msemaji wa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Msemaji Mkuu wa Ikulu ni Greyson Msigwa.
 
Reactions: E84
Msemaji Mkuu wa serikal ni Zamaradi Kawawa.
Msemaji Mkuu wa Nchi ni Mkurugenzi wa Habari Maelezo.
Msemaji wa Rais ni Katibu Mkuu Kiongozi.
Msemaji Mkuu wa Ikulu ni Greyson Msigwa.
Mkuu Pohamba asante kwa ufafanuzi...hawa wote wanapataje hizo nafasi, je wanatuma maombi ama wanateuliwa ? je majukumu yao hayaingiliani?msaada tafadhali.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…