Nadhani upo sawa kwenye polling hakuna jingine hapo, haiwezi kuchukua resources nyingi simply kuangalia kama kuna files mpya, kama kuna mpya unazicopy kuziprocess kisha unazimove katika folder nyingine kuwa zishafanyiwa kazi.
Kuna FileSystemWatcher Class
FileSystemWatcher Class (System.IO) katika .Net ambayo kazi yake ni kumonitor folder for new/changed files sijui unaandika program ya aina gani kwenye .Net ila unaweza kuitumia hiyo hasa kwenye Windows Service application.
Issue ya pili inabidi uwe na njia ya kuidentify file ipi ina format ipi filename ni njia mojawapo so mafile yenye jina linaishia na _Users.xlsx yatafuata format fulani so tumia method hii kuzisoma data.
Kama kuna column names unaweza kujaribu kusoma column name kwanza kisha kama ndo unayoihitaji ukazoma data zake.
Pia kama format inatofautiana kati ya wateja unaweza ukawapa kila mmoja folder yake kwenye FTP then kila mmoja awe ana logic yake kwenye code.
Kama format zinabadilika kila wakati hapo unajitengenezea matatizo makubwa in the end, ni muhimu kwenye software interfaces kati ya systems tofauti ziwe well defined na hazibadiliki ovyo.
Kutegemea na uhahijati kusoma excel files za mwaka gani pia library unazoweza kutumia zinabadilika e.g.
GitHub - ExcelDataReader/ExcelDataReader: Lightweight and fast library written in C# for reading Microsoft Excel files