Msaada ndugu zangu dawa ya kunguni

Hivi ile sumu bado inapatikana kweli siku hizi, nakumbukuka ilipigwa marufuku lakini ilikua kiboko ya wadudu wote wa nyumbani.
Nawashukuru sana kwa ushauri wenu ule wa maana nitaufanyia kazi haraka kwa kweli kunguni ni wasumbufu sanaa
 
Hao wahuni hawaondokagi mpaka ukiwashe,lasivyo wakikuzoea Ndio imetoka.Na kukiwasha namaanisha uchome hayo matandiko kabla hawajakichafua.
 
Dah! Jiandae kupokea harufu mpya ndani ya nyumba yako, maana hizo dawa za kunguni sio poa.
 
Tafuta dawa ya wadudu inaitwa Akheri Powder utawakomesha. Lakini ujue hayo ni maroho ya mizimu ya kwenu yanakushambulia kwa kukiuka masharti ya ibada za kiukoo. Kumbuka kule misri yalitumika na Musa kama mapigo kwa Farao ili atii amri ya kuwaachia wana Waisraeli kutoka utumwani.
 
wana nyanyasa..
 
Kuna dawa flani hivi unga unga wa rangi ya pinki unapakwa kwa kutumia unyoya wa kuku kwny kitanda na godoro aisee hutakuja kuona tena kunguni maisha yako yotee!
 
Kuna dawa flani hivi unga unga wa rangi ya pinki unapakwa kwa kutumia unyoya wa kuku kwny kitanda na godoro aisee hutakuja kuona tena kunguni maisha yako yotee!
Nikisumbuliwa na kunguni Kwa miaka miwili yaani Kila njia na dawa nilitumia lakini walikua waipoa Kisha wanakiwasha. Sasa nilipewa dawa ikiwa kwenye kichupa Kama vile vya dawa za sindano maarufu PPF. Ile dawa ilikua na rangi Kama mafuta ya kupikia na nililipa shilingi elf 15 na matumizi yake ni kupaka Kwa kutumia unyoya Kama hiyo dawa Yako. Nilipaka sehemu Kama sita kidogo kidogo na ilibaki nyingi tu. Tangu hiyo siku mpaka Leo ni miezi sita Sasa sijaona hata kifaranga Cha kunguni.

Sijui dawa inaitwaje maana aliniuzia ikiwa Haina maandishi yoyote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…