Msaada: Ndugu yangu anasumbuliwa na tatizo la kuvimba mwili

Shmaider

JF-Expert Member
Oct 2, 2015
406
120
Nawaomba wataalamu mnisaidie maana ndugu yangu anasumbuka sana viungo mbali mbali ktk mwili wake huwa vinavimba na wakati vinavimba huwa anahisi baridi kali pamoja na maumivu makali.

Hali hii huwa inamtokea mara kwa mara anaweza kuamka kavimba mdomo mara jicho mkono n.k
 
Mpelekeni hospitalini huko mtapewa prescription ya hilo tatizo
 
Nakumbuka kuvimba mwili ni baadhi ya dalili ya Ugonjwa wa moyo kama ilivyowahi kutokea kwa bibi yangu tatizo hili lilimtokea kwa mara ya kwanza akiwa njiani, miguu na mwili wote ukavimba na alikuwa peke yake akashindwa kutembea akalala palepale, walivyompeleka hospital wanasema ni ugonjwa wa moyo.Hata mi lilinitokea Kipindi nipo mdogo ila ilikuwa ni miguu pekee Lakini niliwahi matibabu nikapona
 
Ulitumia dawa zipi
 
Dawa alizopewa haziendani na Minyoo yake, au naweza sema Dawa alizopewa haziendani na Ugonjwa wake.

Cha kufanya,

Bila kupoteza Muda nendeni Hospitali ya Uhakika ili Ndugu yako akapimwe upya, na aangaliwe hizo Dawa alizopewa kama zina uhusiano wowote na matatizo yake.

Yawezekana ni uzembe wa hao waliompa Dawa, wamempa Dawa sizo.

Jitahidini sana kuwahi Hospitalini haraka iwezekananvyo kabla madhara hayajawa makubwa
 
Wewe jamaa kule SIASA wamefuta Uzi wako.

Uzi wako haujadumu hata kwa Dakika Mbili.

Imeonekana wewe ni miyeyusho.

Sababu Uzi wako wa kule na huku ni vitu viwili tofauti.

Kama kweli ulichobandika kule SIASA kuhusiana na Ndugu yako, Jibu ni hilo hapo juu yangu.

Bandiko namba Kumi na Moja (11)
 
Kuna jamaa yangu naye ana tatizo la kuvimba hivyo hvyo haSa sehemu aliyoumia,anavimba haswa ,alienda hosp wakamwambia labda tatizo litaKuwa kwny msukumo waA damu ,nahisi inaHusiana na moyo hapo..ila aLipata tiba kwa lupimo clinic kule geita ,amesema zimemsaidia (no promo,am trying to help somebody) so kama utakuwa vizuri ni vyema Alachua vipimo hosp na pia kwenda kwenye hizi herbal clinic
 
Wewe jamaa kule SIASA wamefuta Uzi wako.

Uzi wako haujadumu hata kwa Dakika Mbili.

Imeonekana wewe ni miyeyusho.

Sababu Uzi wako wa kule na huku ni vitu viwili tofauti.

Kama kweli ulichobandika kule SIASA kuhusiana na Ndugu yako, Jibu ni hilo hapo juu yangu.

Bandiko namba Kumi na Moja (11)
Nahic watakuwa hawajauelewa ila niule ule
 
Nahic watakuwa hawajauelewa ila niule ule
Kiongozi Suala si kutokuuelewa, Suala ni kwamba:-

Kama ule Uzi usingefutwa ningekuwekea hapa na kisha tungepima Mizani, nnakuahidi hata wewe mwenyewe Muhusika Mkuu ungeona tofauti.

Unajua kwanini?

Hapa umezungumzia kuwa Ndugu yako anasumbuliwa na matatizo ya kuvimba Mwilini mwake, ikiwemo na viungo vyake pamoja na maumivu makali.

Uzi uliofutwa ulidai Ndugu yako anasumbuliwa na Minyoo na mkaenda Hospitali mkapewa Dawa za Minyoo, baada ya Ndugu yako kuzitumia hizo Dawa za minyoo tu akaanza kuvimba.

Tukiweka Mizani, jibu ni kwamba:-

Kwa Uzi huu Ndugu yako tatizo la Kuvimba Mwili wake ni la kwaida, amma naweza sema ni Desturi yake Kuvimba Mwili, au naweza sema, ni Ugonjwa unaomsumbua mara kwa mara, nikiwa na maana Ugonjwa huo wa kuvimba haujaanza jana wala leo.

Tukija kwenye Uzi wako uliofutwa SIASA, ni kwamba:-

Ndugu yako alipatwa na Minyoo, mkampeleka Hospitali, akapewa Dawa, na mara baada ya kupewa Dawa ya Minyoo tu, matokeo yake Mwili wake ukaanza kuvimba. Na ukiangalia jibu unapata tatizo la yeye kuvimba Mwili limesababishwa na hizo Dawa alizopewa Hospitalini.

Je hapo kuna mwingiliano wowote wa Mabandiko yako yote mawili?

Je hapo utawalaumu Viongozi waliofuta Uzi wako?

Jibu ni kwamba ingekuwa Uzi wako huu unamwingiliano na Uzi wako ule uliofutwa SIASA, pasi na kipangimizi chochote kile Uzi wako ule uliofutwa SIASA na Uzi wako huu ungeunganishwa.

Kwa haraka haraka umeshindwa/unashindwa kufikiria kitu kama hiki!

Hivi hizo Shule mlienda kusomea ujinga? (Kwa Sauti ya Bibie FAIZA)
 
Back
Top Bottom