Msaada: Nataka kwenda Nairobi

mzeelapa

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2010
Posts
1,124
Reaction score
408
Wana JF sijawahi kufika Nairobi, nataka kwenda kutembea angalau kwa wiki moja, natokea DSM nitumie mabasi gani ambayo yanaaminikaa? Nauli ni bei gani? Ni hoteli gani naweza kufikia kwa mimi wa kipato cha kawada na maeneo gani ya kutembelea? Tahadhari gani nichukue nikiwa huko? Majibu serious tafadhali.
 

Usikose kutembelea huku kwetu Kibera pia
 
Mabasi ya kuaminika panda Dar Express kwenda Nairobi. Kufikia hoteli ambayo utakuwa na uhakika unaweza fikia Kipepeo.
Uwe makini na wakora sawa, pia mabomu kwasasa si unajua Al shabaab hawatabiriki.
Safari njema.
 
Unaposema kwa ww mwenye kipato cha wastani unamainisha nn!? Je Unafikiri kwa Mtoto wa SSB kipato chake akikuambia kipato changu ni cha wastani atakuwa ana-pocketi kiasi gani kwa Mwezi!?

Watanzania bwana, kwa kuficha ficha hatujambo. Be specific kuwa kipato changu ni wastani wa laki mbili hadi 6, au laki 8 hadi 2M ili watu wajue watakushauri hotel gani uende ukastarehe.
 

Kwanza kabla ya yote una passport? Usije ishia mpakani
 
Kwa upande usafiri bus la Dar Express itakufaa.
 
panda mtumbwi.......mpaka nairobi
 
Mabasi ya kuaminika panda Dar Express kwenda Nairobi. Kufikia hoteli ambayo utakuwa na uhakika unaweza fikia Kipepeo.
Uwe makini na wakora sawa, pia mabomu kwasasa si unajua Al shabaab hawatabiriki.
Safari njema.
Kuna thread moja humu ndani wanasema wahudumu wa Dar Expr. wanaboa lakini sijui kwa vipi. Sasa hiyo Kipepeo iko eneo gani au mitafikaje?
 

Kwa hii safari nimetenga Shs.1.0 mil. sitegemei kufanya shopping labda zawadi ndogondogo tu kwa ajili ya jamaa zangu wa karibu, lakini silazimiki.
 
Nikipata mwenyeji nitamuomba anitembeze maeneo hayo, kuna kivutio gani huko?




tumia modern coast upitie zako mombasa kwenda nrb.ni adventure.utayapata dar kwenda msa
 
Nairobi hua tunakwenda kwa ndege. ndege nzuri ni KQ

Mkuu hela yangu yote si itaishia kwenye nauli? Ndio maana nimeomba msaadawa kujua basizuri na nauli, ingekuwa enzi zile za EAR ningepanda, maana lilikuwepo mara mbili kwa wiki DSM-NRB double engine.
 
Nakumbuka hili basi la chini lilikuwa na sehemu mbili second class na third class. Second class ilikuwa mbele kuishia usawa wa mlango wa abiria na kulikuwa kumetenganishwa kabisa, huko wengi walikuwa wakikaa wahindi, wazungu na watumishi wa serikali wenye vyeo au vizito. Huku nyuma (third class) ndio kulikuwa kwa walala hoi, ole wako konda akukute umezamia 2nd class. Lakini Mabasi ya siku hizi ujanja kuwahi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…