Msaada nataka kuua mti

Rihana

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2013
Posts
498
Reaction score
250
Wakuu nyumbani kwangu nina mti mkubwa sana wa mkorosho umekuwa kero sana unaleta wadudu wakubwa kama funza wanashambulia maua yake...nataka kuuangamiza ili hao wadudu wasiendelee kudondoka chini...sina chain saw( ule msumeno wa umeme) je njia gani inaweza kuuwa mti huu haraka bila ya madhara?
 
Mkuu mwaka mzima mbona mbali?
Then nunua chain saw faster kama unaona kuuchuna gamba takes long au kodi watu wa shoka- nguvu siku moja tu mkoroshi chini unatumia kuni zako!
 
mi nakushauri utafute dawa ya kuangamiza hao wadudu,uendelee kufaidi kivuli na matunda ya mkorosho. Mazingira bila miti ni janga.
 
kuua kitu kisichokua na defense machanism huoni kuwa ni dhambi? tafuta dawa hasa mtwara zinatangazwa redion kila siku. kuua sio solution yenye hekima. mti mmoja una uwezo wa kutoa kilo 100 za korosho ghafi na kilo moja ya korosho ghafi ni shi TZS. 1,200 ambayo huwa inalipwa kwa installments. so mbali na kivuli na ku-preserve nature, ukiutunza vizuri huo mti unapata Annual turn over ya tzs 120,000 ambayo itaweza kugharimia kuzuia wadudu waharibifu kuzaliana juu ya mti huo.
 

Mkuu nimeona busara ya post yako..hata hivyo tayari nimekwangua baadhi ya magamba yake sasa sijui utakufa? usipokufa basi sinta ukata tena nibora nitafute dawa!
 

mkuu lakini kuna kitu huwa nasikia wanaita kuvuna misitu, mfano ile nguzo inayoingiza umeme nyumbani kwako bila shaka ni mti uliokatwa, kwa hiyo ni dhambi sana sisi wanadamu tunapata...je wewe unakula nyama ya ng'ombe? au vegeterian? vyote hivyo ni viumbe hai ambavyo mwenyezi mungu alitupa tuvitawale....
labda waliobobea kwenye maandiko matakatifu watusaidie kama kukata mti ni dhambi
 
ukikata kitu chochote kwa maana ya matumizi maalum, basi yale matumizi yanakua yamejustify. unjua Bwana Mungu aliposema though shalt not kill, haku-specify ila at the same time anasema utengeneza hiki na hiki ambacho unakuta kinatokana na vitu fulani ambavyo vingine vilikua hai. kwanza huo mti unaweza kuta watu ndo wameufata ulipo wala sio mti uliowafuata wao. sasa nani anatakiwa kuondoka. nadhani miti pia ni composition nzuri ya kufanya mahali unapokaa pawe lively sio unakua kama umejenga jangwani. utakata mti halafu unakumbana na upepo, jua, exposure. naweza kwenda mbali lakini ni sawa na kufukuza mke ukadhani atakayekuja hatakuwa na kasoro


 
Mwagia petrol,then piga kiberiti,dk 5 tu kwisha kabisa.
 
Mwagia petrol,then piga kiberiti,dk 5 tu kwisha kabisa.
mkuu mimi natafuta njia isiyoweza leta madhara mti huu uko karibu na nyumba sasa mafuta na kiberiti tena huoni ni majanga????
 
mi nakushauri utafute dawa ya
kuangamiza hao wadudu,uendelee kufaidi kivuli na matunda ya mkorosho.
Mazingira bila miti ni janga.

we ndyo umeandika kitu cha maana kuliko wote
 
ondoa gamba kuzunguka kwenye shina, na upake chumvi hapo ulipotoa gamba..then wait for some months
 
Kweli amri ya mungu ya Usiue imenifunga hapa....maana viumbe hai ni pamoja na mimea, maskini huu mti nimeshaukwangua magamba si kwenye shina bali kwa juu kidogo...labda utachipua tena? any ideas?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…