Asante kwa taarifa hii mujarabu mkuu. Basi yawezekana mimi nilipata tiba nusu au robo. Nilimezeshwa dawa ya heligokit ambayo nilikuwa nameza vidonge vitatu asubuhi na vitatu jionii kwa muda wa mwezi mmoja; ikifuatiwa na umezaji wa kidonge kimoja kila siku kwa muda wa mwezi mmoja. Kisha nikaenda kupima nikakuta bacteria bado wapo wa kutosha. Nilipomuuliza daktari imekuwaje sijapona akanambia huenda nimepata new infection. Again nikapewa dozi ya pili kwa mtiririko huo huo. Baada ya kumaliza dozi hii ya pili, nikaenda kupima na kukuta bacteria wapo. Nikakata tamaa na kuamua kubaki na bacteria wangu hadi nitakapopata tiba asilia.
Mkuu, naomba kama kuna hospitali inayotibu ugonjwa huu unielekeze niende nikatibiwe maana hivi vidonda vimenitesa kwa muda miaka 16 sasa (tangu mwaka 2002). Hata mtu akiniambia mavi yanatibu nipo tayari kula ilimradi nipone. Natanguliza shukrani.
huyo mtaalamu wako labda alijichanganya...ukipima H.Pyroli test lazima irudi kuwa positive sababu mwili una antibdoy tayari vs huyo mdudu.
Hivo haishauriwi kupima H.Pyroli test i.e kwa njia ya damu baada ya kumaliza doze yake....inabidi kupima Fecal stool antigen au vpimo vingine zaidi vizuri ambavyo viko very specific kudetermine kama mdudu ametoweka kwenye damu.
Vipimo vingi vya ku check antibody huwa sio vizuri wakati mwingine,ni sawa na ku check HIV antibody test kwa mtoto mchanga alozaliwa kwa mama mwenye HIV/AIDS ukitegemea itakua Negative.(wakati mama anampsia mwanae antibody).Antibody test inaweza kuwa positive na vipimo kama PCR kigawa negative ambacho ndo kipimo sahihi kama unaelewa sayansi nyuma yake.
Na kuwa na H.Pyroli test positive haikuondolei wewe kuwa na vidonda vya tumbo vinavyosababishwa na chanzo kingine.
Hivo ni vema kuwa cautious kwamba kama chanzo kimoja akijapona na dawa umetumia kwa usahihi basi maana yake kuna chanzo kingine na ni rahisi kukitafuta ukionwa na daktari ambaye anafanya kazi kwenye hospitali zenye nyenzo.
Na point ya tatu ya msingi ni kwamba hao wadudu wengi wao nao sio malofa wengi wao wana mutate na kutengeneza resistance dhidi ya dawa...Hivo kuna First,Second and third line ya matibabu...IKigoma ya kwanza maana yake usiendelee kumeza first line inabidi daktari akuhamishie second line na hili ni swala la maarifa ya wataalamu utakaokutana nao kuchanganua hizi hoja tatu na kuendelea kukutibu wao kukupatia rufaa kwenda kwa Gastro-Enterologist maana madaktari wengi wamesoma ile general medicine na kuna maarifa wanakua Shallow na hapo linapokuja swala la kumpatia mtu rufaa aonwe na watu walobobea
Ushauri: Nenda hospitali ya MKoa omba rufaa kwenda kwa Gastro-enterologist hao ndo wamesoma miaka zaidi ya mita wakisomea matumbo tu nje na miaka mitano ya udaktari wa kawaida na nje na miaka mitatyu ya u specialist wa kawaida.
Jumla wamesoma miaka 11 kwenye fani ya udaktari na lazima tukubali kuwa hiyo miaka ya ziada wana kitu cha ziada wanakijua.