Nimepatikana!
Nipo kipindi kigum kuna mimba mwanamke mpenzi wangu ananiambia nimempa na sikutarajia kabisa kwani maisha yangu bado sijajipanga nawaza sana.
Mwanamke ananiambia ye hajui la kufanya ananisikilia mimi. Nawaza nimwambie aitoe ila naogopa sana ni dhambi hiyo ya kuua hata yeye anaogopa.
Kifupi nimechanganyikiwa sana. Aliponiambua tu haoni siku zake na anapata maumivu ya tumbo akiinama roho yangu ilipasuka paah nikabaki nakumbuka ile stori ya Adam na Hawa jinsi Adam alivyokua anamlalamikia Hawa kwa Mungu kwamba mwanamke aliyempa ndo amesababisha yote.
Nitafanya nini nikisema nimlalamikie kwa nini hakujua kama siku tunafanya kale kamchezo ni siku za hatari na yeye atanilalamikia kwanini nilimlazimisha.
Kifupi nimekoma kwa sasa naona ndo akili za kiutu uzima zinakuja na hisia kama nimekuwa mkubwa ghafla. Najiuliza au niikatae hio mimba kama wengine wanavyokimbia ila napata matumaini na maneno ya MAGUFULI kwamba tufyatuane hakuna tatizo.
Vijana wenzangu wa kiume ambao tayari mna watoto ilikuwaje asee mkakubaliana na hali? Kwangu mimi bado nashangaa shangaa. Sielewi kwanza kumbe watu wawili wanaweza kutoa copy ya mtu mmoja.
Nakiwaza hiki kipindi cha ujauzito mpaka atakapojifungua nitampa nini nami bado ni tegemezi hali ya maisha sio nzuri? Niikate hii mimba?Itakuwaje nyumbani kwao wakimwambia aje kwangu(kwetu)?nitaweza kweli kulea ?
Maswali ni mengi sana, yajayo yanafikirisha.