Msaada: Naomba kujua jinsi ya kufika Mafia-Island kutokea DSM

Lyagwa

JF-Expert Member
Feb 3, 2013
1,634
893
Hi, Jf members

Naomba kujuzwa ni jinsi gani rahisi na nafuu ya kuweza kufika katika visiwa vya Mafia nikitokea Jijini Dar es salaam.

Kama kuna usafiri wa boti (Fast ferries) itakuwa vema pia na ni wapi zinapatikana na kampuni husika, na kama ni ndege (Aeroplane) ni kampuni gani na upatikanaji wake (schedule).

Ni muhimu, Ahsanteni.
 
Majahazi tu nenda ferry utapata maelezo pia kisiju ndio yako mengi..Mkuranga huko!kule ndio njia panda ya Mafia!ama la panda vindege vidogo!
 
mbagara rangi 3 panda magari ya nyamisati utapanda boti au mitubwi yenye engine acha uzembe nenda njia panda ya ulaya panda nddge dk 20
 
mbagara rangi 3 panda magari ya nyamisati utapanda boti au mitubwi yenye engine acha uzembe nenda njia panda ya ulaya panda nddge dk 20

Sio uzembe mkuu, ndio maana nimeuliza njia zote na ndege ikiwemo, kwangu swala ni njia rahisi na rafiki ya kufika Mafia kirahisi maana sijui hata uelekeo wake. Je ni kampuni gani ya ndege inafanya safari za Mafia mkuu maana naona unasema ni dk 20 tu, nadhani una uzoefu na unaweza kuwa msaada kwangu, please assist.
 
kitu air tanzania ila ni kuanzia tarehe 25....

ATC kuanzia tarehe 25 ya mwezi gani mkuu, na kama una detail nyingine zaidi kuhusu hao ATC naomba ufunguke zaidi, mfano wanaendea mara ngapi kwa wiki nk.

Ahsante, nasubiri kusikia kutoka kwako mkuu
 
Majahazi tu nenda ferry utapata maelezo pia kisiju ndio yako mengi..Mkuranga huko!kule ndio njia panda ya Mafia!ama la panda vindege vidogo!

Ahsante mkuu, hivi vindege vidogo ni vya abiria ama vinakodishwa, ufafanunuzi tafadhari
 
Kuna ndege 2 kwenda Mafia, Coastal Aviation ndege 2 kwa siku saa 4 na saa 9 na nauli yao ni 120,000Tsh one way, pia wapo Tropical air wao ndege yao inaenda Mafia kila siku saa 4 asubuhi na nauli ni 105,000Tsh one way!

Usafiri wa boti ni kupitia Nyamisati unatakiwa kuwahi Mbagala upande gari za Nyamisati saa 12 asubuhi (nauli 4,500Tsh hadi 5,000Tsh) na pale Nyamisati boti inaondoka kuanzia saa 4 asubuhi nauli ni 10,000Tsh na inatembea kwa masaa manne hadi matano kufika Mafia. Na Mbagala to Nyamisati ni masaa mawili na nusu hivi, ndege ni nusu saa tu!

Karibu Mafia!!!
 
Hakika wewe umekuwa msaada mkubwa zaidi, nakushukuru sana, nitakaribia hivi karibuni.
 
Back
Top Bottom