Nitafanya hivo japo kwa sasa naishi mkoaniNadhani ungeanzia hapo kota... Kota za wanajeshi au polisi then unaenda kambini wanakuwaga na list
HayaNitafanya hivo japo kwa sasa naishi mkoani
AsantePole mwaya...!! Kumkosa baba ni kukosa vitu vingi sana maishani!!!
Habari wana JamiiForum, naitwa Christina umri miaka 28. Namtafuta baba yangu mzazi kwani toka nimezaliwa sijawahi kumuona zaidi ya kuambiwa alipokuwa akiishi na mama yangu alishafariki lakini kabla ya kufariki nikiwa na miaka 12 alinambia kwamba baba yangu alimpa ujauzito wakati akiwa anafanya kazi kama house girl mtaa wa Keko Machungwa kwenye kota na majina sina hakika ila kumbukumbu zangu alinitajia kuwa ni Nyalusi Kikoti. Naomba kwa yeyote ambae atakuwa anafahamiana au anaweza kuniunganisha nae anisaidie kwani haja yangu kubwa ni kumfahamu baba yangu na si vinginevyo. Kwa mawasiliano kuhusiana na jambo hili namba yangu ni 0758905911 hii namba inapatikana whatsapp tu. Mungu awabariki
Hii inanikumbusha dogo mmoja aliwahi kuwauliza ndg wa mama yake alipo baba yake. Ndg wa mama wakaona labda ni kwa sababu ya ugumu wa maisha kijijini, wakaamua kumpeleka mjini.
Huku mjini walimpeleka shule. Huko shuleni alikutana na kijana wakawa marafiki na hivyo akawa anaenda nae kwao. Siku moja walimkuta mama wa rafiki yake, akawa anamwangalia sana yule kijana. Hatimaye alimuuliza jina lake na asili ya baba na mama yake. Dogo akaeleza asili ya mama yake na jina lake ila baba alisema hamjui hana historia yoyote juu ya baba.
Mama wa rafiki yake aliposikia jina la mama wa dogo, akajua dogo ni motto wa kaka yake, kwani alimpa mimba mwanafunzi akiwa kidato cha pili miaka ya 1988 na hasa jinsi dogo alivyokuwa anafanana na kaka yake.
Kwa mtindo huo dogo aliweza kukutana na baba yake.
Mungu huwa akipanga jambo, litawezekana, hivyo nawe jitahidi utampata baba siku moja
Ni wapi huko?Mkuu wewe ni mtu wa nyasirori???