MSAADA: NAMNA YA KUAPPLY KAZI ONLINE SERIKALINI.

Sung

Member
Mar 2, 2019
40
20
Heshima kwenu wakuu.

Naomba kufahamishwa hili maana sijui inakuwa kuwaje.
Hivi ajira zikitangazwa serikalini, njia nyepesi kuApply ni ipi?

Nilipitia site ya portal.ajira.go.tz, nikaona kuna sehemu ya kujaza taarifa (CV) kisha zinaweza tumika kwa kuombea kazi, sasa je hii ndio site inayotumika au kuna njia nyingine?

Mfano, leo serikali ikatangaza ajira labda kwa wahudumu wa afya, steps za kufuata ni zipi?

Juzi kati, kulikuwa na nafasi za walimu, nikasikia malalamiko mengi kuwa mfumo/mtandao unasumbua, ni mfumo gani huo. Ni kwa walimu tu au kwa profession zote?

Natanguliza shukrani.

Wenu Junior,
Sung
 
Njia hutofautiana kulingana na matakwa ya mwajiri.
Kuna hii ya kupitia sekretarieti ya ajira ambayo ni common maana taasisi nyingi huwatumia utumishi kupata watumishi.
Mashirika mengine huajiri wenyewe direct, hapa sasa utafuata maelekezo utakayokutana nayo. Wakikuambia tuma kwa njia hii fanya hivyo.
 
na hayo maelezo huwa wanatoa kwa njia gani?
Maana wengine mtaa umetu-keep busy hata mambo ya nafasi za kazi huwa tunasikia tu kupitia kwa watu wengine, hatujui huwa zinatangazwa vipi tofauti na kupitia tovuti ya shirika husika.
Njia hutofautiana kulingana na matakwa ya mwajiri.
Kuna hii ya kupitia sekretarieti ya ajira ambayo ni common maana taasisi nyingi huwatumia utumishi kupata watumishi.
Mashirika mengine huajiri wenyewe direct, hapa sasa utafuata maelekezo utakayokutana nayo. Wakikuambia tuma kwa njia hii fanya hivyo.
 
Je, naweza ili kuomba kazi, lazima kuwa na transcript mbali na cheti cha taaluma husika? maana nimeona kule tovuti ya utumishi wanataka mtu a-upload cheti husika pamoja na transcript.

Na je mfano, nikiwa na trascript bila cheti napo naweza omba kazi?
 
Ndio ni muhimu kuwa transcript
 
Je, naweza ili kuomba kazi, lazima kuwa na transcript mbali na cheti cha taaluma husika? maana nimeona kule tovuti ya utumishi wanataka mtu a-upload cheti husika pamoja na transcript.

Na je mfano, nikiwa na trascript bila cheti napo naweza omba kazi?
Hautoitwa mkuu Cheti ni Muhimu kuliko Transcript bila Transcript unaweza fanya USAILI ina maana ukiwa na cheti tu pekee ila bila Cheti hutoweza fanya USAILI ina maana ukiwa na Transcript pekee jitahidi upate cheti.
 
Back
Top Bottom