Hilo dogo sana na ni rahisi kupita maelezo,kwanza inata kujiamini na usiwe upande wa kuvunjika moyo ,muhimu kwa vile upo sehemu ingine ,itakuwa ndio ize ,vizuri anza kuzoeana nao mpaka wamekuzoea ,hapo mazoea yakishakuwa hayana wasiwasi chagua target yako na katika mazungumzo mkiwa mpo wengi au yupo na wenzake jaribu kumuunga mkono katika vyanzo vyake vya habari anavyoanzisha au mazungumzoni wala usiwe unamtazama ,ila kitu kimoja mtupie macho ya kawaida yasio na ishara yeyote ila uyatulize kwenye uso wake na jitahidi iwe mnagongana macho ,usigande zaidi ya sekunde mbili ,endeleza hali hiyo mpaka nayeye aanze kuizoea ,hii itamjia automatic wakati mkigongana macho na pia kuwa karibu nae wakati wa mazungumzo ya pamoja na wenzake.
Endeleza mpaka akuzoee kivyake na ajione yupo salama kwani hujamgusia chochote upo katika kuchanganya chemico tu,Sasa anza kupandisha joto ,katika mazungumzo ya pamoja ikiwa mwenzake hayupo muulize yyeye kwa kumwita jina lake fulani fulani yupo wapi ,akikujibu (ni lazima akujibu) endeleza mazungumzo kwa kuliizia huyo mwenzake ,labda atakujibu sijamuona,muulize mbona hujamtafuta mwenzio ,pengine anaumwa yaani umzungumzishe japo dakika tatu inne ,nia yako ni kujenga mahusiano ya karibu zaidi ,pia ukishaongeza mahusiano hayo ,sasa anza kuchimba shimo hapa unaweza kumuuliza suala lolote lile ,mfano unaweza kumwambia nyumbani wanataka kujenga nyumba lakini hawajui kuipanga jiko lipo wapi ukumbi waweke wapi una idea yeyote ile ? Kama una kalatasi ni vizuri zaidi na pencel ila baada ya maneno mawili matatu kupita kama ana ushauri atakupa na ridhika na oneza kuwa amekupa ushauri mzuri. Jingine kama unatafuta stori ,unaweza kuona paka au kuku au bata au mbuzi au ng'ombe ,jidai kushtuka nae kwamba umeona kitu labda ukamwambia mtizame yule ,atakuuliza kwani ana nini ,utamwambia nyumbani mlikuwa nae kama yule ukimpenda kwelikweli lakini aligongwa na gari basi ametuhuzunisha sana nyumbani ,unaona eei ,kisha unamgeuzia yeye suali hilo kwani wewe mnapenda nini ,usitumie unapenda nini ,tumia mnapenda nini .nyumbani kwenu au mna mifugo ,hapa unatafuta kuuteka moyo wake na kudumisha ajione yupo na mtu anaejali,hii inakuwa ndani ya moyo wake,hivyo ukifanikiwa kwa hayo atakuwa kwanza hawezi kukukosa kukuona ,kumbuka hujamtajia kitu kuhusu mapendo ,saaaaaaaaasa ukishaona kazoea ,jaribu kumpima ,kivipi ? Anapokuwa na wenzake penda kuzungumza na wenzake na sasa usimtazame tena ,cheka nao changamka nao zaid hao wengine katika mazungumzo ya kawaida tu ,kama ameanza kukupenda atanyamaza kimya atakuwa hasemi na anaweza kuondoka hapo kwani utakuwa unajua kinachoendelea.