Msaada: Nahitaji leseni ya udereva

Msaada: Nahitaji leseni ya udereva

Joined
Mar 10, 2015
Posts
17
Reaction score
0
Habari za asubuhi wapendwa,

Naomba kujua ili kupata leseni ya kuendesha gari daraja lolete lile natakiwa niwe na vigezo gani na ni kwa kipindi gani na ni shilingi ngapi?

Please
mnijuze
 
Habari za asubuhi wapendwa!

Naomba kujua ili kupata leseni ya kuendesha gari daraja lolete lile natakiwa niwe na vigezo gani,na ni kwa kipindi gani,na ni shingapi?? plz

Kwa kuwa wewe ni mara yako ya kwanza kujifunza kuendesha gari inabidi uanze kujifunza kuendesha magari ya Class D. Na ili uweze kujifunza na kupata Leseni lazima ufuate hatua zifuatazo:
  1. Kwanza kabisa nenda TRA ukakate TIN namba.
  2. Baada ya kukata TIN namba kata na ulipie Leseni ya Learner hapo hapo TRA na gharama yake ni TZS 10,000/-
  3. Kisha nenda kwenye shule ya udereva yoyote utakayopenda ukajiandikishe na kulipia mafunzo yako ya udereva ambayo yanachukua mda usiopungua wiki 4 na gharama yake haizidi TZS 300,000/-. Usisahau kwenda na leseni yako ya learner maana hutaruhusiwa kujifunza kuendesha gari bila leseni ya learner.
  4. Ukishahitimu mafunzo yako ya udereva na kupata cheti utatakiwa kwenda kufanya mtihani ili uweze kupata leseni yako ya Class D. Taratibu za kuufanya mtihani huo utapewa huko shuleni ila utatakiwa ulipie TZS 3,000 TRA kama gharama ya mtihani.
  5. Kama ukifaulu mtihani wako utawekewa PASS na utaambiwa uende TRA na leseni yako orijino ya learner ukalipie leseni yako ya Class D na gharama yake ni TZS 40,000 ambayo ina expire baada ya miaka 3.
 
Aisee umeelezea vema sana ndugu. Shukurani sana kwa niaba ya madereva njuka wenzangu.
 
Back
Top Bottom