Msaada nahitaji kuiagiza gari nje ya nchi

Madam vivian original

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
503
990
Wakuu habar za weekend,

Ndugu yenu nimejichanga nataka na mimi nimiliki gari na hii ndo mara yangu ya kwanza kumiliki usafiri.

Nimeona kabla sijafanya maamuzi nije kwenu wakuu mnishauri mawili matatu, bajeti yangu ni m16 na gari niitakayo au niipendayo ni Nissan dualis, au Suzuki escudo.

Naombeni ushauri juu ya hz gari mbili changamoto zake, na kama mngenisaidia kampuni nzuri ya kuagiza gari au hii pesa yangu naweza pata gari gani ukiacha IST.

Msaada wenu wakuu nisije nikaingizwa mjini jamani.

Sent from my Infinix X683 using JamiiForums mobile app
 
Be forward, kwa mtazamo wangu ni kampuni nzuri japo zipo nyingi kama SBT Japan n.k. Ngoja wadau wengine waje wakupe miongozo zaidi
 
Madam vivian original

Nikupongeze kwa kujichanga, ili Mimi na wadau wengine hapa tuweze kukupa mwanga mzuri kabisa wa haswa gari ipi ambayo itakufaa, ukizingatia kwamba umesema ndio mara yako ya kwanza . (Bila kujali una experience au la)

Ninaweza kukushauri juu ya Dualis sawa, kwa sababu ni gari nzuri kweli kwa wanawake haswa wa kileo, ulaji mzuri wa mafuta.

Lakini,

Tunaweza sema chukua Dualis, kumbe unakaa sehemu za ndani ndani huko ambazo njia ni mbovu , sehemu ni ya milima, kipindi cha mvua utelezi

Sehemu gari inapokua inakwenda (go and return) daily ni mbali , idadi ya watu ni kubwa.

Trust Me, utakuja hapa kutulaumu wadau kwamba tumekushauri uchukue gari ambayo sio nzuri kwako.

Kumbe ni maelezo yako hayakuwa yamejitosheleza.

Tungependa utuelezee vizuri machache yafuatayo ili wadau waje kukupa muongozo sahihi zaidi.

1. Gari itakapokua inatumika zaidi
2. Umbali wa matumizi ya kila siku
3. Watu wanaopakiwa kila siku (Idadi)
4. Hali ya barabara ya itakapokua inatakiwa kupita kila siku.

Hayo ni machache ya msingi kati ya mengi, ambayo naamini ukiweza kufafanua vyema basi itakuanrahisi kupata ushauri mzuri wa gari bora kabisa itakayo kufaa.

Nawasilisha.
 
Back
Top Bottom