Msaada: Mwenye kufahamu hili

TODAYS

JF-Expert Member
Apr 30, 2014
14,599
23,886
Najipanga kusafiri kuelekea nchini Swaziland kwa mfalme muswati, mwanaJF amabaye anaweza kunipa muelekeo wa safari na jinsi ninavyoweza kutumia garama ndogo, ikiwa no usafiri pamoja maisha ya hapo Swaziland.

Nawasilisha.
 
Chukua fastjet mkuu mpaka johannesburg then ukifika airport chukua tax meter kama rand 400 mpaka johannesburg park station hapo ndio stand kuu ya mabasi ya nje ya nchi na mikoani..kwa muda utakaofika baada ya masaa matatu mbele utapata basi la Swaziland ni kuanzia rand 400 kuendelea mpaka 600 basi zuri zaidi kwa basi sio mbali kutoka Jozi ni kama masaa ma tano tuu..nunua rand au us dollar yote sawa tuu..ila unapokuja kwa madiba usisahau vaccination card wanasumbua oliver tambo hata beit brigde pia..change kwa ss ipo rand 15.75 kwa us 1..uwe makini sana huko kwa mswati ukishindwa mkuu tumia kinga wana migongo sana harafu wamejaa magonjwa na pia hawakatai appointment...fastjet wapo cheap hii season cheki nao mapema mkuu..hotel ni rand 300 mpaka 500 johannesburg na swazi hawapishana sana..izo za kawaida kwa watalii zipo za bei zaidi ya hiyo ni wewe unataka ipi
 
Kata tiket ya return ya kurudi Tanzania pia upandie hapo oliver tambo kama ukiweza unaweza book kulula.com wapo cheap pia wanaenda swaz ukifika oliver tambo unakata hapo hapo kama hautaki kusafiri kwa basi..ila basi zao zipo vizur ni greyhound au Intercape utauliza izo kampuni woote wapo sawa hao ukipanda hata usafiri mrefu hauchoki...
 
Isanga family
Comrade nashukuru sana umenipa wazo la mwanzo ambalo nalifanyia kazi.

Ila unaonesha mwenyeji sana location hzo mpaka kujua issue ya migongo doo!! - Asante.
 
Ok poa kata mapema tkt ya fastjet ni laki tano tuu mpaka jozi na kurudi dar..chakula kuna nandos,chicken liken,kfc na zingine nyiingi tuu gharama zao rand 50 na kuendelea inategemeana na chakula unachotaka...ratio ya migongo ni 10 kwa mwanaume mmoja hapo kwa mswati ukienda mkuu leta mrejesho...kama Botswana tuu..poa maandalizi mema ya safari yako..
 
Basi kutoka dar mpaka Tunduma utalipa tsh 45,000 utalala tunduma hotel tsh 15,000 kesho yake utachukua basi Tunduma mpaka Harare kama tsh 80,000 Taqwa bus unafika Zimbabwe siku inayofuata saa kumi jioni ukifika hapo kituoni..utaenda kuoga wanakofikia hao madereva wa Taqwa ukisubiri chakula utachelewa kupata bus la Pretoria hapo shukia pretoria uchukue basi la Swaziland..Harare to Pretoria rand 300 mpaka 400..na pretoria to Swaziland rand 300 pia izo gharama mm nikijumlisha na siku kama tatu ivi naona inazidi laki tano ya fastjet ya kwenda na kurudi panda ndege mkuu uokoe muda pia..basi tunapanda kama tunarudi na mizigo mikubwa au tunarudi na gari za kaburu ambazo zinalipika kodi maana huku magari mengi bei za kawaida bei halisi ya gari unaipata Tunduma mkuu..
 
Ila pia unaweza ukapanda basi kutoka Tunduma mpaka lusaka ukifika Lusaka unalipa kama $ 70 basi la shalom au jordan mpaka jozi moja kwa moja ukifika unachukua basi la swaziland sema hayo mabasi ya Zambia hawafiki park station utakapofika chukua Tax mpaka park station usitembee kwa mguu na beg lako Jozi kuna Wakabaji wanajiita MDU NA HAO PANYA ROAD WALIOKIMBIA BONGO WANAKUFA TUU HAPA MAANA WANAWAKABA HATA WAIOKABIKA MATAX DRIVER WANAOTEMBEA NA BUNDUKI NA VISU...JOZI KUTEMBEA MUDA SALAMA NI SAA MBILI ASUBUHI MPAKA SAA KUMI NA MOJA JIONI KWA WAGENI kwa hiyo take care mkuu..
 
Mkuu kama utapita zambia waombe wale jamaa wa mabasi ya kitanzania wachenji iyo hela ya kizambia kwatcha maana wengi hawazijui ukichenji mwenyewe unaibiwa unapewa pungufu sana..hayo ni malalamiko ya kawaida Tunduma kutapeli wasafiri..chenji kama ya kula tuu unapopita Zambia kama 50k baki na dola na Zambia utakata tkt kwa dola ukisema uchenji Tunduma ujanja ujanja kama hazijui kwatcha zao..
 
Nitafanya money exchange hapa hapa town bongo kwenye bureau de change ili kuokoa ulanguzi. Nahisi kutumia bus naweza kuwa na utalii mzuri njiani kupitia hiyo miji au? Isanga family
 
Ok poa mkuu yaa ukitembea na basi uta enjoy pia but ili usichoke ushuke Lusaka uanzie pale usipitilize hadi Harare..Shuka Lusaka panda Bus za Jordan au Shalom ni iriza Q i 7 leather seat pia very confort..kila boarder unapofika ugonge na Chirundu ni ofisi moja wazambia huku wazimbabwe kule gonga kote na Wazim waambie upo Transit to Swazi ukifika south usiseme upo transit utapewa siku chache anakuuliza unataka siku ngapi mwambi 2 weeks ukipita kwenda swazi zimeisha hata ukikaa siku moja kwa madiba ila unaporudi unafanya ivyo ivyo.utakaposhukia na basi za kizambia ndio utapopanda wakati wa kurudi mtashukia kerk street/nugget st unapotoka swazi ufike mapema hapo mtaani hotel za kulala zipo hapo kuna Tivol hotel na Vip ipo juu kule but better ulale tivol ni cheap na wafanyabiashara wakizambia na Watz ndio hulala hapo asubuhi unawahi basi lako kwa mguu tuu ni kama mita 250 mpaka katika basi lako...usipande basi moja linaitwa Cr lusaka ni zuri but wanasumbuliwa mara nyingi beit bridge boarder wanabeba viatu vya mtumba kutoka Tz na chakula bila vibali kwa iyo muda mwingine linazuiliwa mpaka shift ibadilike ya custums officer..all in all Nakutakia safari njema mkuu..naenda mtaani mkuu kama una swala lingine ni mpaka nirudi usiku..mimi narudi home Tanzania jumatano hii ningekupokea vizuri tuu na tukijaaliwa ntakua huku tena 20 march tutawasiliana pia..
 
Na kama unataka kurudi Tz kutoka huku panda Shalom basi kuelekea Lusaka pitia victoria falls bei ni moja usipande la chirundu ss iv maji yapo mengi pale na watalii wa kumwaga mtakaa na basi kama masaa matano iv ni boarder ya kuingia zambia vtu vyao vyoote hushusha chini kwa ajili ya ukaguzi..utalipia rand 50 tuu kwa ajili ya kutembea na rand 10 wana sehemu za kuoga kwa kulipa watalii ni vyoo visafi na vizuri vipo standard..chakula usile hapo boader mtatoka hapo na basi mpaka livingstone utaulizia ofisi za Shalom hapo sio mbali wanachoma samaki wakubwa sana na ugali kwa hela ndogo tuuu.. I wish u all the best..
 
jamaa umetoa maelezo mazuri sana. hata mimi nimeelewa. shukurani sana,ngoja niandae safari ya kwa madiba
 
Comrade Isanga family asante sana, umemaliza yote nadhani, but now najikusanya nione safari ianze lini.
But yote kwa yote ukirudi joh nitaku_check mkuu.
 
Naona Mkuu Isanga family ametoa majibu yote, kikubwa hebu jipange kabla hujataka kuianzisha hiyo safari yako. Naamini kila kitu kinawezekana Mkuu.
 
Back
Top Bottom