Msaada- MUHIMU

Kirachacha

Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
67
Reaction score
48
Wasalam.

Mimi ni mdada naishi Arusha na nnasoma chuo,ada najilipia na nina mtoto mdogo. Nna msichana wangu wa kazi anaetokea Busaka iko Chato Geita. Huyu binti aliishia form 2 baada ya kukosa ada. Japo alikuwa na nia ya kusoma mazingira ya kwao ni magumu. Kwenda shule ndo abahatishe, hata akienda shule nyumbani hawezi kusoma, yeye na wadogo zake ndio wakafanye vibarua nyumbani wapate kula.

Mimi nilivyomchukua nia yangu ilikuwa anisaidie kumwangalia mwanangu wakati mimi nasoma, akikuwa kidogo na mimi nikimaliza chuo nimpeleke akasome QT au hata kozi fupi tu ili na yeye ajipatie ujuzi utakaomsaidia mbeleni, hilo halijabadilika.

Kinachofanya nije kwenu ni kwamba ana mdogo wake ambae licha ya kwamba wazazi walimwambia asije akafaulu maana hawawezi kumsomesha alifanya vizuri na akapata nafasi ya kwenda form 1 huko huko kwao. Tangu januari hajahudhuria shuleni mpaka wazazi walipoanza kusumbuliwa na mgambo. Sasa leo wamempigia huyu dada yake (binti yangu)wakitaka atume pesa ya ada. Alivyoniomba ushauri nimeshindwa kumwambia moja kwa moja kama atume au la maana yeye mwenyewe ana wasiwasi kwamba anaweza akajikamua akatuma mshahara wake lakini ikawa kazi bure. Wingi wa kazi, kukosa mwanya wa kujisomea nk vikafanya asipate chochote shuleni.

Sasa nafikiria kumsaidia ila nahitaji support kidogo.
Naweza kumchukua nikae nae pamoja na dada yake nimtafutue na shule. Kama kuna yeyote anaeweza kuniunga mkono kwa msaada wa hali, mali au mawazo ntashukuru sana. Kwa atakaependa kujua zaidi awe huru kuniuliza kwa PM, mawasiliano zaidi naweza kutoa baadae.

Ahsanteni.
 
ungetupa mchanganuo wa mahitaji ili tujue tunafanyaje.
 
Mdogo wangu, pole kwa habari za kupiga shule na wakati huo huo kwa kulea mwanao mdogo pamoja na msichana wako wa kazi. Pia nakupongeza sana kwa moyo wako wa upendo na nia njema ya kutaka kusaidia huo ukoo. Simaanishi kukukatisha tamaa, ila naona nikushauri kama kaka endapo hautapata support ya kipesa au vitu vidogo vidogo kama ulivyoomba. Kwa kifupi, niseme mchango wangu ni wa mawazo kama ifuatavyo ...

Kwa kifupi sana ni kuwa katika dunia hii huwezi kumsaidia kila mtu wala kumpendeza kila mtu. Maadamu uliamua kumsaidia huyo msichana unayekaa naye, ni vyema ukaendelea naye huyo ili usijikute una mzigo mzito wa kusomesha kuliko uwezo wako. Ni bora ukajitahidi kumsaidia huyo uliyenaye na kisha ku-concentrate na masomo yako ili ufanye vizuri huko chuoni kuliko ku-coordinate makusanyo ya hela na hivyo vitu vidogo vidogo kwa ajili ya hiyo familia. Naamini wasamalia wema kama wewe wanaweza kujitokeza kwa yule mdogo wake.

Sina nia mbaya, ila niko concerned na maisha yako binafsi na pia nina hofu na masomo yako ktk kipindi hiki huku ukikabiliwa na zoezi la kulea mwanao mdogo. Ni hilo tu.

Samahani kama mawazo yangu yatakuwa yameenda kinyume na matarajio yako au ya wana JF wengine.

Wako,
HP.
 
::
Hao wa Busaka,Buziku,Bwanga,Buseresere,Buzirayombo n.k Nawapata vema Kwa ushauri wa kifikra tu ni huu
::
WEMA UKIZIDI UWEZO NI DHAMBI.
=
 
Jaribu kutafuta mashirika yasiyo ya Kiserikali, Ustawi wa Jamii, Ofisi za Mkuu wa Mkoa n.k nina imani huko waweza kupata msaada kwa urahisi.
 
atume tu kwa kua kafaulu ajitahidi kumtia moyo asome , ada ya serikali dada yake anaweza imudu , asome akiwa huko kwao, mazingira magumu hayaepukiki la msingi amjenge kisaikolojia tu kua anahitaji kwenda extra mile
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…