Msaada: Mtunzi wa sauti toka Ughaibuni ndg. Christopher Mwashinga

Msaada: Mtunzi wa sauti toka Ughaibuni ndg. Christopher Mwashinga

Emanzi

JF-Expert Member
Joined
Oct 13, 2011
Posts
261
Reaction score
118
Naomba msaada wa kupata mawasiliano ya mtunzi wa sauti toka Ughaibuni, mashairi ya matumaini ndg. Christopher Mwashinga.

Kama yumo humu anipm namba nimpigie ni muhimu.
 
Mimi namfahamu, ni Mchungaji wa kanisa la wasabato, na mkewe ni rafiki yangu sana, Nina namba ya mkewe, but I don't know how to send private messages, I don't see that option
 
Inaonekana ni muda mrefu huu uzi haukujibiwa. Leo nimepata Jibu, Mwandishi wa Kitabu hicho cha mashairi, kiitwacho "Sauti Toka Ughaibuni" hatimaye nimefanikiwa kufika kwenye Duka ambalo vitabu vyake vinauzwa pale kwenye jengo la Mwembechai Plaza magomeni. Nilishangaa kuona vitabu vingi vilivyoandikwa na huyu mwandishi. Kilinivutia Kitabu chake kikubwa cha mashairi, chenye mashairi zaidi ya 800 kiitwacho "Tumaini lenye Baraka" Kwahiyo basi, wewe uliyekuwa unatafuta mawasiliano ya mchungaji huyu nenda pale Magomeni Mwembechai Plaza Dar es salaam, duka linaitwa "Maximum Hope Bookshop"ukishindwa kwenda kama upo mbali nitakutumia jumatatu kwani ninampango wa kwenda kununua vitabu vya mashairi, kwani napenda sana mashairi yenye muonjo WA kiroho kama anayoandika mchungaji Christopher R. Mwashinga. Jr. Usiku mwema wanajamii forum, ngoja nilale zangu
 
Back
Top Bottom