Msaada mtoto wangu hataki kula

Nuoxian

Senior Member
Mar 15, 2020
169
237
Kama nilivyoeleza hapo juu, mtoto wangu wa kike umri ni mwaka mmoja na miezi 4 amekuwa akigoma kula na kama akila basi ni kidogo sana napo hadi umlazimishe.

Tatizo linaweza kuwa nini? Na suluhisho la hili tatizo ni nini?
 
Mkuu acha tuu huo umri ndo wenyewe yani Unaweza ugua kichaa...Mwanangu alikuwa hali na akila anatapika dadekii..!!
 
Mchanganyie Unga wa mlonge kwenye juice hata akinywa nusu glass inatosha. Kijiko kidogo cha chai kwenye glass ya juice au maziwa
 
Mchunguze anaweza akawa na meno ya plastic, huwa yanawasumbua sana watoto

Hayana shida yoyote meno ya plastiki.

1: Watoto hawa wanaweza kuwa na shida nyingine ya kiafya.

2: Wakati mwingine ni tabia kulingana na umri.

3: Wengine ni mtindo wa maisha: tunaeapa maziwa na juice zenye sukari nyingi kitu ambacho huwafanya wawe na shibe na nguvu za kutosha na wadione haja ya na hamu ya kula.

NB: Wahusishe wataalamu wa afya kujua nini kinamsibu mwanao.


View: https://www.instagram.com/p/CoROgx0t6oX/?utm_source=ig_web_copy_link
 
Back
Top Bottom