Msaada: Msingi wa nyumba

dada dori

JF-Expert Member
Mar 26, 2015
233
93
Habari wana JF,

Naomba msaada kwa wazoefu&wataalamu wa ujenzi wa nyumba kuhusu msingi wa nyumba.Je ni kweli msingi wa nyumba ya matofali ya kuchoma huwa unajengwa kwa kushindilia mchanga tu na kupanga matofali bila zege na nyumba ikadumu?

Naomba msaada wenu&mbarikiwe.
 
Hiyo itakuwa si nyumba ya kudumu ama hali ya uchumi iwe hairuhusu maana watu wanajengaga nyumba ya udongo kila kuanzia chini hadi juu...Ila kama mtu unataka kujenga sidhani kama kuna fundi mwenye uwelewa anaweza kukujengea nyumba imara kwa njia hiyo ulioiainisha...
 
ZEGE MUHIMU MKUU. KAMA UNAANZA NA MATOFALI YA KUCHOMA CHINI HAKIKISHA ENEO HILO HALINA ULE UDONGO WA NGUSERO KAMA NJIRO ARUSHA, YAANI UNAKATA AU KUPASUA NYUMBA.

NIMEONA WATU WAKIANZA NA TOFALI ZA KUCHOMA CHINI.. KONDOA, BABATI, KITETO N.K. ILA HUKU NI KICHANGA SANA.
 
unaijengea ukanda gani, tukupe soil characteristic ya ukanda huo ndio ujue msingi unakuwaje!?
 
Asanteni sana kwa msaada wenu.Nyumba najengea maeneo ya morogoro
Nakushauri uwe makini sana na ushauri unaopokea hapa jukwaani, wapo wachache wanafahamu ujenzi na walio baki wanachangia kwa mazoea hasa walivyoona au kusikia ujenzi ulivyo. ikiwa utachukuwa kila ushauri utahombana na fundi wako bure.
kwangu mimi naona fundi wako anajua anachokifanya na inaelekea eneo/site yako ni ya mfinyanzi ndio maana anatanguliza mchanga japo hii njia inahitaji mjuzi sana na angejengea tofali za kulaza za 6" kwasingi wote ndipo walling ndo ajengee matofali ya kuchoma...hii ingekupa matokeo mazuri zaidi.
wengi wamezoea kumimina zege chini japo wengi wao hamudu gharama, wanabana matumizi na matokeo yake humlazimu fundi kumwaga zege dhaifu.
 
  • Thanks
Reactions: Mss
Hiyo itakuwa si nyumba ya kudumu ama hali ya uchumi iwe hairuhusu maana watu wanajengaga nyumba ya udongo kila kuanzia chini hadi juu...Ila kama mtu unataka kujenga sidhani kama kuna fundi mwenye uwelewa anaweza kukujengea nyumba imara kwa njia hiyo ulioiainisha...
mkuu bila shaka huna uzoefu na ujenzi.
njia hii ipo hadi ulaya japo inahitaji umakini mkubwa sana.
tukianza kuelezana kiundani namna ya ujenzi wa misingi, wengi wetu tunaweza kuelewa kuwa tumezoea tu aina flani wa ujenzi wa misingi na isivyo sahihi
 
Nimeona nyumba nyingi zikijengwa na tofali za kuchoma, na wanajengea udongo mwanzo mpaka mwisho except linta ndo zege lake wanatumia cement, na wanasema zinakaa muda mrefu zaidi kuliko matoli ya kuchoma!

ukisemaa ujengee cement btn blocks itakula kwako manake matofali ni madogo cement itaenda nyingi zaidi ni bora ujengee tofali za kawaida tu ujue moja! then fence utajenga kwa tofali za kuchoma
 
Nyumba ni msingi, ukikosea unaharibu nyumba yote. Hiyo yako sijawahi kuisikia
 
Ni hivi,fundi anasema kuwa msingi sio lazima niweke zege,ameshauri kuwa msingi ukishachimbwa ashindilie mchanga halafu aanze kuweka tofali.Zege niweke kwenye linta.
 
Ni hivi,fundi anasema kuwa msingi sio lazima niweke zege,ameshauri kuwa msingi ukishachimbwa ashindilie mchanga halafu aanze kuweka tofali.Zege niweke kwenye linta.
Msikilize fundi anasema nini mimi si mwenyeji wa huko morogoro lakini kuna ndugu yangu anaishi ifakara nyumba yake nayo ilijigengwa kwa mtindo huo nadhani wenyeji wa huko wanauzowefu na huo ujenzi wa aina hiyo.
 
Ni hivi,fundi anasema kuwa msingi sio lazima niweke zege,ameshauri kuwa msingi ukishachimbwa ashindilie mchanga halafu aanze kuweka tofali.Zege niweke kwenye linta.
Mimi pia fundi wangu kanishauri nisimwage zege nichimbe mzingi halafu nishindilie mchanga kisha nijengee tofali za block kama coz tano kisha niendelee na tofali za kuchoma. Naombeni ushauri pia wana JF najengea Dodoma
 
Back
Top Bottom