Wapendwa wanajf.
Habari za mda huu. Nnaomba kwa yeyote anaefahamu anijuze.
Mimi natarajia kujiunga na chuo mwaka huu na nmepata mkopo kutoka bodi ya mkopo, kinachonisumbua ni hiki. (1)hizo fedha ntazipata kwa njia gani na wakati hawana accaunt no. yangu? (2)chuo cha private ntasajiliwa bila fedha?
chuo chocchote huwezi sajiliwa bila pesa unless uwe umepata mkopo 100%,otherwise kua mpole acc no mtaandika chuoni.
ONYO- usiifanye hiyo pesa ka pombe allowance
masomo mema
Utakapofika chuoni,baada ya kufanya usajili utaandika account no. Yako ambayo itatumwa na chuo chako kule bodi ya mikopo. Na tatizo ni kuwa karibu vyuo vingi vinalazimisha mwanafunzi kulipa nusu ya ada ndipo apate usajili. Sasa hilo ni suala lako na chuo. Ila hata kama unapata 100% ada itakapotumwa utakuwa na haki ya kudai kurudishiwa kile kiasi ulicholipa hapo mwanzoni.
Kwani hukujaza acc. no. kwenye form wakati wa kuomba huo mkopo?
Sioni kama inaleta maana ukishafika chuo ndio utumiwe hela, je kama huna hata kianzio na umepata 100%??!!
Anyway, kwa nchi hii chochote kinawezekana!!