Allah's Slave
JF-Expert Member
- Mar 14, 2008
- 562
- 46
Mkuu mshukuru Mungu huyo mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke. Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7 years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.
Kwani huko nyumbani ndio kuzuri?
Unafikiri akikaa nyumbani ndio yuko safe?
Tafakari.
mtafutie mke mwenzake!
Mkuu mshukuru Mungu huyo
mke wako anakutunzia watoto wako na wewe anakutimizia mahitaji kama mke.
Huko maofisini unakotana kumleta mke wako si kuzuri, kuna mambo mengi
tunayaona na kuwafanyia wake za watu yasiyostahili. Kama hana munkari wa
kazi au biashara au shule haina maana ni mke kilaza. Tafuta kitu
atakachofanya kitakachokuwa na interest kwake. Lakini usimhukumu after 7
years, lazima kuna mazuri uliyaona kwake. Wewe ndio baba na kidume
kwenye familia, kutunza familia ni jukumu na wajibu wako. La msingi
waandalie mazingira mazuri wanao endapo Muumba ataamua kukuita mbele ya
haki wangali wadogo. Tusifananishe wake zetu na wake wa marafiki zetu
kwani hujui wao wanaumiza vichwa kwa lipi.
pole sana slave. nafikiri uchaguzi ndio umekuangusha.huenda uliangalia sura yake nzuri (naasume tu maana ndio tabia zao). Hata hivyo, ni vema ukae nae na kumweleza umuhimu wa yeye kufanya kazi.pesa ulizonazo asidhani kuwa ndio amefika.itakuwaje leo ukifilisika? si atakukimbia atafute mwingine mwenye hela? ya mung mengi , japo siombei...kesho na keshokutwa 'ukamaliza kazi yako hapa duniani', ataishije? na kwa baadhi ya familia na koo, kama ukatangulia, wazazi na ndugu za mume humpokonya mali zote kwani wanajua kuwa wewe ndiye mzalishaji.atafanyeje? mweleze ukweli wote ili auone huenda akabadilika.pole na ninakuombea katika hilo.
mume anakupa laki tano kwa wiki kazi unafanya siku nzima unalipwa laki tano na makato juu neti laki 3 ...kwa nini nifanye? nani hapendi kula bata dunia hii?Na wewe anza kumdanganya kwamba biashara haiendi mambo yamekuwa magumu hela ambayo huwa ya matumizi ambayo huwa unampa anza kumpa nusu yake ili ajue kwamba maisha ni magumu ataanza tu kujishughulisha
umeona eeh tena huyo mke wa pili unamfungulia biashara ya maana ! akiona mwenzake anastawi atashtuka!wangu umenena... ndio dawa! jamaa aoe mathna!
kaa na mkeo .mweleze jinsi anavokukera na kukuchosha na hayo maisha yake! labda hajui kama yupo wrong as long anakula na kushiba.
kama ulishamweleza hakukusikiliza na kubadilika basi wewe cha kufanya achana nae fanya mambo yako kama hayupo vile!