Msaada mke mjamzito na ana tatizo la kupungua kwa damu

Wild fauna

JF-Expert Member
Apr 22, 2012
461
189
Salaaam jf
Naomba ushaur na msaaada wa mawazo kwenu mke wangu ana ujauzito wa karibu week 32 sasa.

Ameenda hospitali na akaambiwa ana tatizo la damu na wakamwambia inabidi afanye utaratibu wa kuongeza damu kwa kula mboga mboga. Pia wamemwambia kuhusu juice ya rozela.

Ningenda kupata ushaur zaidi, ni vitu gani haswa vinaweza kumwongezea damu kwa haraka? Hii juice ya rozela inatumikaje?
Naomba kuwakilisha
 
matembere. Juice ya Rozela, Fruto ya Ribena, pia kuna dawa ya kuongeza Damu inauzwa kwenye Maduka ya Dawa.

Mnunulie Mkewako, na pia uwe unamsimamia Azingatie kunywa maana wakina mama wenye ali hiyo wanahitaji kuangaliwa sana.

Maana wengi wao hawanywi ukiwapa kisogo, hivyo ni vyema ukawa karibu nae azingatie kunywa.
 
Nashukuru mno kwa ushaur
 
Nashukuru mno kwa ushaur

Mnunulie matunda yaitwayo beet roots yanapatikana kariakoo shimoni mara ya mwisho nilinunua kilo moja tsh 7000/= mwambie aoshe, amenye maganda vizuri halafu asage juisi yake mwambie achanganye na asali kidogo anywe kila siku. Atumie hiyo juisi siku saba tu. Anywe muda wote kama juisi nyiginezo ila isilale awe anakunywa ikiwa freshi itamsaidia sana
 
Aoshe matembele vizuri,ikiwezekana Na maji ya vuguvugu,asage Hayo matembele,Ile juice anayopata ainywe..ni ngumu lkn inasaidia kweli...
Kwa Umri wa mimba alionao pls kuweni makini sana khs swala la damu..
 
Beetroot, Makomanga (juice), Tende saga na maziwa, Matembele na hizo mboga za majani, na pia vipo vidonge vya kuongezea damu, na nina wasiwasi wakati wa mimba tangu awali hakuwa akinywa vidonge vya folic hivyo ni vizuri wakati wa ujauzito. Kwahiyo tumia hizo juice uloambiwa na vidonge mana muda ulobaki ni mchache sana ufanye hivyo kwa pamoja kwa matokeo ya haraka.
 
Azingatie ushauri uliotelewa na wadau hapo juu. Tembele, Rozela etc.

Mtoto anakuwa na anahitaji damu ya kutosha na mama yake pia. Huu ndo mda wenyewe otherwise atazaliwa na damu kidogo afu itaanza kusumbua.

Damu inatakiwa iwe kati ya 9-13.
 
Looh, fanya haraka uhakikishe anapata hizo mboga na juice kwa kiasi kikubwa kabla hajajifungua, hakikisha madaktari wanajiridhisha, nakumbuka mwaka 2007 nilimpoteza my aunt kwa sababu hiyo, alijifungua baada ya siku 8 akafariki na kuacha kichanga, kwa kukosa damu..was painfull to us na tulipata mengi ya kujifunza!!
 
Nitachukua tahadhari mjumbe. Mungu ni mwema,
 
Nashauri vile vile ahudhurie clinic aonapo shida yeyote. Anyway, huo ujauzito ni wa ngapi? Ana history ya kutoka damu nying anapojifungua?
Kaka jipange upate mtu wa kumuongezea damu kuanzia sasa, kwani chochote kinawezatokea from now.
Azingatie ushaur hapo juu, vile vile hata maharage yanahusika kuongeza damu.
 
Beetroot mwisho wa matatizo....

Aivumilie ilivyo mbaya

Atengeneze juice fresh anywe asubuhi mchana jioni usiku

Anywe kadri awezavyo
 
Beetroot mwisho wa matatizo....

Aivumilie ilivyo mbaya

Atengeneze juice fresh anywe asubuhi mchana jioni usiku

Anywe kadri awezavyo
mbaya kweli ila ni nzuri sana ukitaka pia kujipima kama una maradhi unatakiwa unywe ile fresh ukikojoa damu ujue una shida
 
mbaya kweli ila ni nzuri sana ukitaka pia kujipima kama una maradhi unatakiwa unywe ile fresh ukikojoa damu ujue una shida
Hapana ile huwa si damu (unless iwe damu damu)

Kawaida ukiila sana mfululizo lazima mkojo na haja hubadilika rangi.....
 
Mchicha unauchemsha kidogo na nyanya nyingi akiweza afanye ndiyo mboga yake ya kila siku, mwekee budget hata ya nusu kilo ya nyama ya ng'ombe kwa siku, akimaliza kula supu ya nyama ale machungwa straight away.
 
Inshu ya dam ni very sensitive kwa mjamzito mkuu,so dedicate time kufuata ushauri zaidi sana jua group la dam yake na jua at least watu watano wenye group sawa in case of emergency una uhakika utawapa,hasa wakati wa kujifungua make sure dam ya ziada iko karibu,usisubiri ya kutoka blood banking,meanwhile fuata vyakula wamevyopendekeza wadau
 
Back
Top Bottom