Msaada Microcontroller

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
2,604
Reaction score
6,756
Wadau naomba kufahamishwa bei za microcontrollers 8051 series na wapi zinapatikana hapa Dar.
 
Wadau naomba kufahamishwa bei za microcontrollers 8051 series na wapi zinapatikana hapa Dar.

MKuu, ulifanikiwa kupata hizo microcontrollers? Kama bado, nijulishe nifanye mchakato.
 
alpha 1, na mim nataka jifunza programing maana sijui hata kidogo, vp nianzaje il niwe na ujuz huo
 
alpha 1, na mim nataka jifunza programing maana sijui hata kidogo, vp nianzaje il niwe na ujuz huo

Mkuu, kwani unachukua kozi gani kwa sasa?
Njia rahisi ni kujiunga na chuo kinachofundisha computer programming,na kozi zote za electrical, electronics, telecommunication, engineering, computer science na IT wanafunafundisha hiyo kitu.

Au kama unataka kujifunza nyumbani bila kwenda chuo,hii ni ngumu sana,itabidi utafute tutorials ujifunze mwenyewe,ila inagharimu muda. Kwa sasa kuna tutorials nyingi kwenye internet ambazo unaweza kusoma na kupata idea juu ya computer programming. Google programming language unayotaka kujifunza upate materials, uanze kujifunza.

Kama lengo lako ni kujifunza Embedded Systems, nakushauri ujifunze C Programming Language,maana ina compilers nyingi za embedded systems ambazo unaweza kuchagua unayotaka.
 
asante mkuu
 
mkuu mm nasomea education, apa ruco iringa
 
mkuu mm nasomea education, apa ruco iringa
Mkuu, kama uko chuo na unachukua kozi ambayo haihusiani na hayo masuala, itakuwa ngumu sana kwako. Labda subiri umalize masomo yako. Lakini kama unaweza, waone watu wa kozi hizi hapo chuoni kwako,watakusaidia: Bsc in Computer Science Information System, Bsc in Computer Science Software Engineering au Bachelor of Accounting and Finance with Information Technology
 
Hizo mavitu watu wanaochukua eletronics ndo wanasoma deep hizo makitu.
Ila akiwa msingi mzuri wa c language itamrahisishia.
 
jifunze assembly language

vitu kama:

set A, 0x23
out A
 
jifunze assembly language

vitu kama:

set A, 0x23
out A

Hapana mkuu aanze assembly hata c hajagusa si ataona nyota nyota. Nadhani ajifunze kwanza c language ambayo inaeleweka then atumie compilers. Akisha master huko mwanzo ndo aitafute assembly yenyewe yenyewe.
 
ok mkuu, kama ni beginner c programming itamfaa sana.
 
Hizo mavitu watu wanaochukua eletronics ndo wanasoma deep hizo makitu.
Ila akiwa msingi mzuri wa c language itamrahisishia.
Ni kweli Mkuu, ila hata akijifunza computer programming hasa C Programming Language, bila kusoma electronics in deep bado anaweza ku-program microcontroller, maana hayo mengine yaliyobakia ni rahisi kama ana-deal na project ndogo-ndogo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…