Ongea nao tu, wataondoka. Pia unaweza kuwa uanwafukiza kwa ubani mara kwa mara.
Unajuwa siri hata ya Makanisani kufukiza ubani? Hususan kanisa katoliki? Ni simple kabisa, haina maana yoyote kiimani, kwanza ni manukato, pili nifuumigation, wadudu wengi hawapatani na harufu ya ubani, ni zoezi lililokuwa likifanyika kukimbiza wadudu.
Hata Waislam walikuwa wakikaa kwenye visomo vyao wanafukiza ubani ili kukimbiza wadudu, na kuwe na harufu nzuri. Majama wengine walipoona wakaona ni ibada ndipo ikashika mpaka leo, lakini ukweli ni kuwa hakuna ibada yoyote ya kufukiza ubani zaidi ya kukimbiza wadudu na kupata harufu nzuri. Iwe msikitini iwe kanisani iwe majumbani.
Mie huwa nafukiza ubani nauchanganya na udi nanyunyizia na banagi kwa mbaaaali, ooh, harufu ya kipekee na wadudu hata mbu hakai.
Fanya hivyo. Lakini usiniige mimi kutumia bangi, usije ukashikwa Tanzania huko. Huku nilipo bangi kidogo ni rukhsa.