Msaada: Matibabu ya homa ya nguruwe

nyabhera

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2011
Posts
669
Reaction score
737
Naishi Mwanza.

Shida imenianza tarehe 3/04/2026. Alianza mmoja hali anasinzia akatapika nikamchinja kesho yaka akaanza wingine nikamchinja.

Kukapoa kama siku 4 hivi.

Leo tarehe 08.04. 2026 mmoja mwenye mimba imetoka pia alikua mchovu tangu jana. Wawili wadogo wamekufa ghafla

Naona vita ndiyo imeenza rasmi. Nina nguruwe kama 80. Wakubwa 18 wengine waadogo miezi 3-5

Naomba kujua kama Kuna namna hata yakupunguza makali ya ugonjwa asante

Asante
 
Daaah pole kwa changamoto.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Huo ugonjwa Hauna Tiba wala Kinga kwa Sasa.

Kupunguza makali, Unashauriwa kuchinja Nguruwe wakubwa woote walioko shambani na kutafuta soko.

Narudia, Acha mawazo ya kutaka kuwatibia au kuwakinga, ni kuongeza hasara zaidi.
 
Kwa siku 4 nimepoteza kwa kifo Nguruwe wakubwa 4. Nimechinja wenye dalili 5. Solo hakuna limepolomoka vibaya jitihada zangu za miaka 3 zinakufa mbele ya macho yangu. Nabaki na madeni tu nilitegema kulipwa nikivuna kundi wa wadogo around July. Nashukuru Mungu Kwa kila jambo. Amen
 
Huo ugonjwa Hauna Tiba wala Kinga kwa Sasa.

Kupunguza makali, Unashauriwa kuchinja Nguruwe wakubwa woote walioko shambani na kutafuta soko.

Narudia, Acha mawazo ya kutaka kuwatibia au kuwakinga, ni kuongeza hasara zaidi.
Nimepokea
 
Pole sana mkuu ! Kama ulivyoshauriwa hapo, suluhu ni kuwachinja tu ..... bora uuze kwa hasara walau uokoe kiasi cha pesa !!! Hii inanikumbusha kipindi flan 16/17 hapo nilikuwa nafuga kuku..... unakuja bandan unaokota kuku 20/30 wamekufa, then zaidi ya 50 wanasinzia ! Ni headache
 
Anza kuuza mmoja mmoja
 
Pole sana Mkuu
Najua unapitia kipindi kigumu sana maana anakuja mnunuzi anakuambia akupatie 100k ukiangalia ni Nguruwe mkubwa kama kilo 100+
Sasa chukua salimia ile dawa ya kuchua alafu weka kwenye chakula kama matonye mawili ivi au umwaga kwenye sakafu itapelekea nguruwe kupiga chafya ivyo itafungua mfumo wa upumuaji na kupunguza idadi ya virus
Jitaidi sana usafi Mkuu Kwa wale ambao Bado wazima
 
Afu nyinyi wafugaji mliofiwa na nguruwe ndio mnawauzia wauzaji wa nyama za nguruwe za mitumba za kona ya bwiru pale watu mpaka tunakula mishikaki ya nguruwe wa kuchoma mpaka 500 mshikaki tena mkubwa๐Ÿ˜๐Ÿ˜ kumbe ni nguruwe wenye homa๐Ÿ–• ndio maana mpaka siku hizi sidindishi vizuri wife anasema niko chini ya kiwango kumbe ni mishikaki ya nguruwe ya kona ya bwiru washenzi nyinyi
 
Hawa wadudu SUA wamewashindwa

Msihangaike na huu mfugo mtakula hasara tu huu ni ukweli unouma
 
Chinja ndugu,huku Moshi ilitokea mwaka Jana mwezi wa saba ilikuwa ni baadhi ya maeneo ,tena wahi mapema kuuza kuokoa pesa
 
Wape magadi, pia wapake oil wazima na mwagia oil kuzunguka mabanda
 
Ulizembea kuwapa chanjo ya kideri
 
ChatGPT imejibuโ€ฆ
Pole sana โ€” hii ni hali ngumu sana hasa ukiwa na nguruwe wengi hivyo. Dalili ulizoeleza (kusinzia, kutapika, uchovu, mimba kutoka, vifo vya ghafla) zinaashiria ugonjwa hatari unaoweza kusambaa haraka kwenye banda lote.





Nitakusaidia kwa hatua za HARAKA za kupunguza madhara wakati ukitafuta msaada wa kitaalamu.














โš ๏ธ Magonjwa yanayowezekana








Kutokana na dalili zako, yanaweza kuwa:












๐Ÿ‘‰ Lakini ASF ndiyo ya kwanza kushukiwa kwa sababu:





  • vifo vya ghafla
  • mimba kutoka
  • kuenea haraka
















๐Ÿšจ HATUA ZA HARAKA (FANYA SASA)








Hizi zinaweza kuokoa waliobaki:








1. Tenga wagonjwa mara moja








  • Weka nguruwe wote wanaoonyesha dalili sehemu tofauti
  • Usiruhusu wachanganyike na wazima
















2. ZUIA kabisa movement








  • Usiuze nguruwe
  • Usinunue wapya
  • Usiruhusu watu kuingia/kutoka hovyo







๐Ÿ‘‰ Hii ni muhimu sana kama ni ASF














3. Usichinje kwa kula au kuuza








Najua tayari umechinja baadhi, lakini:





  • Usile wala kuuza waliokufa au wagonjwa
  • Inaweza kueneza ugonjwa zaidi
















4. Safisha na disinfection








Tumia:





  • dawa kama Jik (bleach)
  • au dawa za mifugo (Virkon, iodophor)







Safisha:





  • banda
  • vyombo vya chakula
  • viatu kabla ya kuingia banda
















5. Tupa mizoga kwa usalama








  • Zika chini kabisa (angalau mita 1.5)
  • Au choma moto
  • Usitupe ovyo
















6. Chakula na maji safi








  • Hakikisha maji ni safi kabisa
  • Acha kuwapa mabaki ya chakula (hasa ya nyama)
















๐Ÿ’Š Kuhusu MATIBABU








Ukweli mchungu:





  • Kama ni ASF โ†’ HAINA TIBA
  • Antibiotics hazitibu virusi, lakini zinaweza kusaidia secondary infection kidogo







Unaweza kufanya tu:





  • kuwapa vitamini (kuongeza nguvu)
  • maji safi muda wote
















๐Ÿ“ž HATUA MUHIMU SANA








Wasiliana HARAKA na:





  • Afisa mifugo wa wilaya (Mwanza)
  • Au kituo cha mifugo karibu







๐Ÿ‘‰ Hii ni muhimu kwa sababu:





  • ASF ni ugonjwa wa kuripotiwa kisheria
  • Wanaweza kusaidia kudhibiti isisambae zaidi
















๐Ÿ”ด Ukweli wa muhimu








Kama ni ASF:





  • Inaweza kuua hadi 90โ€“100% ya nguruwe
  • Njia pekee ni kuzuia isienee
















๐Ÿง  Ushauri wangu wa moja kwa moja








Usichelewe:





  1. Tenga wagonjwa sasa
  2. Funga banda (no movement)
  3. Piga simu daktari wa mifugo leo
  4. Anza disinfection













Kama unataka, niambie:





  • Je wana homa?
  • Ngozi imebadilika rangi (nyekundu au bluu)?
  • Wanaharisha damu au la?







Nitaweza kukusaidia kuchambua kwa usahihi zaidi na kukupa hatua za kulinda hao 80 uliobaki.
 
Kaka kama ulikuwepo Jana kuna Nguruwe wangu mkubwa sana ana nzao 3 hapungui kg 90 (Nyama) ukitoa utumbo na mafuta. Namuita jamaa ananiambia bei gani mimi nikasema anipe angalau 500k, yeye ananijibu ana 100k. Kidogo nimtukane baadae nilipata wa 230k nikachukua kwa bei ya soko la kawaida nilistahiri TSH 800k Kwa bei za hapa.
 
Haya buana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ