msaada madaktari

AnnaG

Member
Feb 28, 2016
37
33
Habari zenu wa ndugu, naomba madaktari mnisaidie. Mimi ni mjamzito wiki ya 23 mtoto wa kwanza nilimzaa kwa operation na alikaa wiki 2 tu akafa. Sababu niliambiwa njia ilifunguka hadi cm 6 ikagomea hapo hapo hadi wakaamua kunifanyia upasuaji. Baada ya mwanangu kufaliki nimekaa miaka 2 ndo nimebeba tena ujauzito. Je, naweza kujifunza kawaida? Au lazima tena operation? Maana napendanijifungue kawaida. Msaada please
 
Pole sana hapo kwanza inabidi ukapime mapema sab ilitakiwa ukae miezi 6 nivyema ukaenda hospital ukapata ushauri na vipimo kama ultrasound
 
Inawezekana, Hakikisha unahudhuria clinic, ikiwezekana clinic za Private.
 
  • Thanks
Reactions: 247
wahi CLinic mapema na onana na Specialist. Yeye atakupa ushauri mzuri baada ya kukupima, uzazi siku hizi unasumbua so nivema upate ushauri kwa mtaalamu baada ya kuonana ana kwa ana.
 
Nenda clinic haraka na uwaeleze kila kitu na pia kutaka kujua kama una uwezo wa kujifungua kwa njia ya kawaida au itabidi iwe C-section tena. Hongera mama mtarajiwa.
 
Nimeenda mpenzi, ila Dr kanambia lazima nipasuliwe huku alivonipima ultrasound alisema kizazi kipo vizuri na mtoto naye yuko vizuri
 
Labda nikujibu tu kwa kitaalam unaweza kujifungua kwa njia ya kawaida au pia unaweza usijifungue kwa njia ya kawaida percentage ni 60kwa 40 huwa client au mteja anayeingia ktk ujauzito tunamuita client kwani ujauzito sio ugonjwa lakini yawezekana ukapelekea kuwa mgonjwa
Huwa tunakitu tunajiribu madoctor km unaweza kujifungua km kwa njia ya kawaida
Huwa tunakulaza week moja au mbili kabla ya edd yako ya kuja kujifungua kukuangalia na kukuweka ktk obsevation ili kujua km utajifungua kwa kawaida
Sifikii sana eti private km walivyokushauri watu huko juu waweza jifungua kwa kawaida ila govmnt hospita huwezi
Haliingii akili ht kidogp lkn km ni mimi naweza kukushauri ukajifungulia ktk hospitali kubwa bila ya kuangalia kuwa ni private au govmnt mfano muhimbili kujifungua mahali km pale ni kuwa kwanza kuna maspecialist wazoefu mbili wako wengi ht ikitokea kuwe na uhitaji wa kushirikisha specialist wawili au watatu ni rahisi kuliko private kwani watakuwa wadogo tu hivyo kufanya ufanisi upungue muhimbili inaandamwa lkn kizuri chochote lazima watu wakiandame na ukiona unaandamwa ujue unatoa huduma nzuri kikubwa tafuta bima nenda clinic onana na madoctor wakutibu km mgonjwa wabima utapewa specialist wazuri na kukushauri na kukuweka under observation nzuri tu
 
Inawezekana, Hakikisha unahudhuria clinic, ikiwezekana clinic za Private.
Sidhani kama ni mtizamo mzuri sana,Clinic zote za private na za umma Huduma zake inategemea na uwepo wa wataalam wazuri na wazoefu ktk kada husika na pia uwepo wa vifaa vya uchunguzi na Huduma pia.
 
Labda nikujibu tu kwa kitaalam unaweza kujifungua kwa njia ya kawaida au pia unaweza usijifungue kwa njia ya kawaida percentage ni 60kwa 40 huwa client au mteja anayeingia ktk ujauzito tunamuita client kwani ujauzito sio ugonjwa lakini yawezekana ukapelekea kuwa mgonjwa
Huwa tunakitu tunajiribu madoctor km unaweza kujifungua km kwa njia ya kawaida
Huwa tunakulaza week moja au mbili kabla ya edd yako ya kuja kujifungua kukuangalia na kukuweka ktk obsevation ili kujua km utajifungua kwa kawaida
Sifikii sana eti private km walivyokushauri watu huko juu waweza jifungua kwa kawaida ila govmnt hospita huwezi
Haliingii akili ht kidogp lkn km ni mimi naweza kukushauri ukajifungulia ktk hospitali kubwa bila ya kuangalia kuwa ni private au govmnt mfano muhimbili kujifungua mahali km pale ni kuwa kwanza kuna maspecialist wazoefu mbili wako wengi ht ikitokea kuwe na uhitaji wa kushirikisha specialist wawili au watatu ni rahisi kuliko private kwani watakuwa wadogo tu hivyo kufanya ufanisi upungue muhimbili inaandamwa lkn kizuri chochote lazima watu wakiandame na ukiona unaandamwa ujue unatoa huduma nzuri kikubwa tafuta bima nenda clinic onana na madoctor wakutibu km mgonjwa wabima utapewa specialist wazuri na kukushauri na kukuweka under observation nzuri tu
Asante kwa ushauri na kunitia moyo
 
Nenda clinic haraka na uwaeleze kila kitu na pia kutaka kujua kama una uwezo wa kujifungua kwa njia ya kawaida au itabidi iwe C-section tena. Hongera mama mtarajiwa.
Thanks alot
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Okay pole. Nilitaka kukupa tahadhari na hospitali za private ni hatari. Vyema Mhimbili kwa sasa
Muhimbili hiyo unayoenda saa 10asubuhi unaitibwa saa 9 jioni? Hakuna hospitali zenye usumbufu kama muhimbili

Private sio zote ni mbaya Mkuu, Ila ukipata private nzuri huduma ni ya haraka na unajaliwa sana..

Labda sijui wewe ulikuwa unaongelea hatari gani?
 
Hospital gani nzuri za private ambazo zinafaaa?na zimeweza kuwasaidia watu??
 
Hospitali zote za Private haujaona hata moja au unataka nidondoshe list? Au mkuu wewe toka umezaliwa haujawahi kutibiwa private hospital? Kama umewahi basi anza na hiyo
 
  • Thanks
Reactions: 247
Habari zenu wa ndugu, naomba madaktari mnisaidie. Mimi ni mjamzito wiki ya 23 mtoto wa kwanza nilimzaa kwa operation na alikaa wiki 2 tu akafa. Sababu niliambiwa njia ilifunguka hadi cm 6 ikagomea hapo hapo hadi wakaamua kunifanyia upasuaji. Baada ya mwanangu kufaliki nimekaa miaka 2 ndo nimebeba tena ujauzito. Je, naweza kujifunza kawaida? Au lazima tena operation? Maana napendanijifungue kawaida. Msaada please

Jibu la haraka ni huwezi kujifungua kwa njia ya kawaida kwa sababu :
  • Unapojifungua kwa njia ya upasuaji inabidi ukae angalau miaka 2 ili kidonda kipone ndio unakuwa na uwezo wa kubeba mimba na kujifungua kwa njia ya kawaida.
  • kidonda cha upasuaji chenye umri chini ya miaka miwili tunakiita "fresh scar" na ukibeba ujauzito kuna risk ya kuweza kufunguka sehemu ya mshono mimba inapokaribia mwisho hasa kipindi cha uchungu.
Kwa kuhitimisha kidonda chako ni kibichi inabidi kwenda kliniki mara kwa mara na watakupanga siku ya kujifungua kwa upasuaji maana hutakiwi kusubiria uchungu.
 
Back
Top Bottom