Msaada: Maana ya ndoto hii

OgaBoy
 
Ndoto hazinaga maana yeyote ok labda kwa wachache humaanisha

Ndoto yeyote ukihadithiwa utaona ina tafsiri tu hata mtu akitunga "nimeota nimeona mawe makubwa kuna maji yanamwagika" ukiwaeleza watu watasema sijui hayo maji yanaamisha kushuka kwa maisha yako sijui bla bla kibao
 
Shida ni kwamba watu wanafuata kanuni ukishasema ni ndoto, watu watachambua ulivyovitaja kwa kutumia kanuni za kiroho na kimaono.Kama unadanganya ni wewe na udezi wako.Kama ilivyo hesabu na ndoto zina hesabu zake.
 
Ndoto yako inashiria upo gerezani ukisubiri chakula, jihadhari usifanye makosa utaenda gerezani
 
Yeee!! Niliwahi ota napaa, na halafu chini kuna watu wakawa wananikimbiza, ni kundi la watu, nikaja kupaa nikaenda mpaka juu ya mti mrefu, kule pia nikakutana na Nyoka walikuwa wamekufa wote, yaani ukitikisa tawi, yanaanguka. Ni noma
 
Na hii ndio maana halisi ya ndoto hiyo.
 
Ahsante sana kwa ufafanuzi.

Niliwahi kuota ndoto kama hii, tulikuwa tupo kwenye foleni ya msosi ikulu, nilikuwa kama mtu wa 3 hivi, ilipofika zamu yangu, Rais wa nchi wa wakati huo alikuwa amekaa table yenye msosi akanizuia kupakua msosi huo (ilikuwa nyama) akaniambia kwa ishara nikae pembeni ya foleni, waliofuata nyuma yangu walipakua msosi. Nilibaki mnyonge sana. Ndoto hii asubuhi nilipoamka niliikumbuka vyema kabisa. Sikuipata maana yake.
 
Daaaah!! Ikuluu
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…