Msaada: Laptop yangu aina ya Dell, imekata moto ghafla

mamitod

JF-Expert Member
Joined
May 20, 2015
Posts
914
Reaction score
385
Jambo wakuu.

Naomba msaada wenu wakuu. Jana nikikuwa nafanya kazi kwenye kilaptop changu DELL lakini cha zamani kidogo. Ghafla kikakata moto. Hakukuwa na power interruption maana kuna vitu vingine pia vilikuwa kwenye umeme. Wandugu naomba anayejua shida ni nini anisaidie.

Kwa kweli ni kama mtu amenikata mikono maana ilikuwa inanisaidia katka kutafuta riziki. Mimi ni mjane sijaajiriwa na hiyo ndio ilikuwa inanipatia chochote cha kuendesha life hapa town. Huwa naandika short stories kwa watoto wa level ya primary. Nimemwandikia pia publisher mmoja vitabu 2 vya English for primary schools, Mungu akipenda vitaanza kutumika mashuleni next year.

Sijaweza kusimama mwenyewe ndio maana bado nawatumikia watu. Naomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na hili. Mwenye computer ya ziada anaweza kunifanya dumping pit yake jamani. Chonde chonde nimepigika, hebu nisaidieni kuokoa hili jahazi. Files zangu zote zimefia humohumo.

Naomba wale wenye kejeli na madharau wakisoma hapa wakaushe tu wasiniongezee machungu.

Nasubiri huruma zenu wakuu. Ahsante
 
hio laptop haikai na chaji? ilianza kuwa haileti umeme au ilikuwa na chaji ikazima ghafla?
 
fanya uchunguzi kwenye adaptor. inawezekana adaptor au charger yake imeungua. kama ni hivyo utalazimika kununua adaptor nyingine
 
Jambo wakuu.

Naomba msaada wenu wakuu. Jana nikikuwa nafanya kazi kwenye kilaptop changu DELL lakini cha zamani kidogo. Ghafla kikakata moto. Hakukuwa na power interruption maana kuna vitu vingine pia vilikuwa kwenye umeme. Wandugu naomba anayejua shida ni nini anisaidie.

Kwa kweli ni kama mtu amenikata mikono maana ilikuwa inanisaidia katka kutafuta riziki. Mimi ni mjane sijaajiriwa na hiyo ndio ilikuwa inanipatia chochote cha kuendesha life hapa town. Huwa naandika short stories kwa watoto wa level ya primary. Nimemwandikia pia publisher mmoja vitabu 2 vya English for primary schools, Mungu akipenda vitaanza kutumika mashuleni next year.

Sijaweza kusimama mwenyewe ndio maana bado nawatumikia watu. Naomba msaada kwa yeyote aliyeguswa na hili. Mwenye computer ya ziada anaweza kunifanya dumping pit yake jamani. Chonde chonde nimepigika, hebu nisaidieni kuokoa hili jahazi. Files zangu zote zimefia humohumo.

Naomba wale wenye kejeli na madharau wakisoma hapa wakaushe tu wasiniongezee machungu.

Nasubiri huruma zenu wakuu. Ahsante

Je! Hukuimwagia kimiminika chochote kwenye hiyo laptop? Kama ndiyo, ujue kuwa kunashort circuit imetokea ndani ya laptop na kama sio...
Chakufanya, jaribu kucheki kama tatizo ni adapter ya computer kwa kutafuta adapter inayoingiliana kwenye hiyo laptop, na kama bado haioneshi mabadiliko yoyote yale; itabidi ibadilishwe power supply (SMPS) ya ndani ya hiyo laptop maana itakuwa na shida.
Na endapo kama utakuwa na haraka katika kukamilisha documents zako zilizo ndani ya computer...itakubidi uchomoe hard disk na kuitumia kwenye computer nyingine kama utaweza kuazima na unaweza ukaiweka kwenye pc nyingine kwa machaguo mawili ambayo ni kuifanya iwe ni external harddisk au kuichomeka moja kwa moja ndani ya pc na baada ya hapo utayatafuta mafile yako na kuyaendeleza kufanya vitu vyako.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom