Msaada: Laptop aina ya Compaq CQ56 haiwaki inaishia kuunguruma

ashomile

JF-Expert Member
Mar 1, 2017
2,661
2,512
Habarini za Asubuhi wakuu,

Wakuu mimi nimeletewa Laptop ukiwasha inanguruma tu feni ila kwenye kioo haoneshi kitu chochote nifanyeje wadau ?

Na huyu jamaa anasema kwamba alikuwa anatumia window 7 lakini baada ya huo window kutopokea updates akaamua kuhamia kwenda window 10 na alivyohama haikuwaka tena.

Laptop inaonekana imewaka mpaka kwenye power ON kuna mwanga.

Kutokana na maelezo yake jamaa alisema hivi,
Nanukuu: Nilipeleka kwa jamaa mmoja akapiga window ndo ikawa haioneshi chochote . Ukiwasha inaunguruma tu.

Hata ile ya kuwashia inaonesha imewaka ila ndo haifanyi kazi.

Nikaombe Ushauri kwenye group moja la Whatssap na nikaambiwa niunganishe external monitor ila nimefanya hivyo bado haiwaki.

Baada ya kupewa ushauri wa kuconnect external monitor nilifanya hivyo kama inavyoonekana kwenye picha hapo chini.

Hatua ya kwanza nimechukua VGA cable kutoka kwenye dekstop nikaihamisha na kuweka kwenye laptop , lakini bado haiwaki na hatua ya pili nimechukua VGA kutoka kwenye monitor na kuunga kwenye display ya laptop lakini mambo bado ni hola . Haiwaki ila inaunguruma tu.

Hiyo ni hatua ya kwanza.

Hatua ya Pili ni hii.
VGA Kutoka kwenye CPU kwenda kwenye laptop lakini bado haiwaki ila huku mashine inaunguruma tu.
Kama inavyoonekana kwenye picha.

NAOMBENI MSAADA PAMOJA NA USHAURI , MIMI NIMEISHIA KATIKA HATUA HIZO.

IMG20210127075027.jpg
IMG20210127075033.jpg
IMG20210127075353.jpg
IMG20210127075401.jpg
 
Mkuu hivi kama logo ya kampuni huioni ukiwasha tatizo ni nini haswa
Kwamba inaweza ikawa ni Tatizo la hardware, logo ya kampuni ikitokea Unaweza access mambo mbalimbali ya kuifanya diagnosis kabla operating system haijaboot kama bios, na diagnosis tools nyengine za kampuni husika, Pia inamaanisha Unaweza ukaboot os nyengine.

Ila kama haitokei ina maana Tatizo ni kubwa zaidi inabidi ufungue machine unanze trial and error.
 
Kwamba inaweza ikawa ni Tatizo la hardware, logo ya kampuni ikitokea Unaweza access mambo mbalimbali ya kuifanya diagnosis kabla operating system haijaboot kama bios, na diagnosis tools nyengine za kampuni husika, Pia inamaanisha Unaweza ukaboot os nyengine.

Ila kama haitokei ina maana Tatizo ni kubwa zaidi inabidi ufungue machine unanze trial and error.
Mkuu kama nilivyoeleza hapo juu naomba upitie uzi wangu yaani nimejaribu kuunga external monitor lakini bado haioneshi kuwaka.
 
I have a similar problem with my Macbook, doesn't boot. Fundi wa uhakika unampata wapi Tz hii?
 
Back
Top Bottom