Msaada kwenye tuta kuhusu Vodacom, TCCIA, Maxmalipona DSE.

sirluta

JF-Expert Member
Nov 28, 2012
6,325
2,486
Mwaka Jana nilinunua hisa za kampuni ya TCCIA kupitia m-pesa. Nikatumiwa SMS ya uthibitisho toka vodacom na DSE kuhusu muamala huo. Nimekaa zaidi ya miezi sita nasubiri cheti cha umiliki wa hisa bila mafanikio. Nikaamua kufuatilia vodacom wanakiambia niende maxmalipo, maxmalipo wakawa wanafanya mawasiliano na TCCIA ili nipate hicho cheti kwa muda mrefu bila mafanikio na wakaamua kusurrender na Mimi nilichoka kwenda maxmalipo kila Mara ikabidi nitafute mawasiliano na TCCIA na nikapata namba zao nikawasiliana nao wakaniambia nitume anuani zangu ili wanitumie hicho cheti. Baadae wakasema kwenye list ya vyeti walivyo navyo hakuna chakwangu hivyo wakaniambia niende vodacom. Nilienda vodacom, kule vodacom wakanipa namba za simu za DSE ili niwasiliane nao. Nikawasiliana nao wakasema niwatumie zile jumbe nilizotumiwa wakati nimenunua hizo hisa, nikawatumia wakanieleza wanafuatilia na nikawa nawakumbisha, zimepita zaidi ya wiki mbili majibu sahihi sipati ndipo wakaja kunitumia namba za simu za maxmalipo tena ili niwasiliane nao.

Hivi ndivyo biashara za kibongo zinafanyika na kw a staili hii uchumi utakua kweli? Nishaurini plz niende tena maxmalipo ama nowafanyeje hawa watu?
 
Back
Top Bottom