Msaada kwenye servers

edneltz

Member
Joined
Jan 14, 2018
Posts
44
Reaction score
25
Habarini wanajamiiforums,Nilikuwa ninashida moja nilikuwa nimetengeneza server kwa kutumia virtualbox server yenyewe ni ya Ubuntu servers,

sasa shida ni kwamba IP niliyoweka kama IP ambayo watu wa nje waweze kuaccess ile server ni 192.168.43.1 lakini mtu wa nje akiaccess haiwezi fungus, lakini nikifungua hiyo address kupitia computer yangu ambayo ni parent ya hiyo sever inaonesha content ambazo nataka zionekane.

Nimefuatilia wanasema sababu ni kwamba hiyo IP ni private IP natakiwa nipate public how can you help me?
 
baadhi ya ISP apa tz wanakupa izo public (ikiwa static) kwa tozo flani
 
Kwanza hiyo IP 192.168... ipo kwenye private range haitakuwa accessible nje ya network yako, ndo maana wewe unaweza ukawa ma 192.168.43.1 na mimi naweza nikawa na hiyo hiyo kwenye network yangu bila kuwa na tatizo lolote kwa kuwa zipo local kwenye network zetu.

Pili hauwezi kujipa public IP address mwenyewe fikiria kila mtu angeweza kujipa address anayotaka ingekua fujo tupu.

ISP wako anakupa public IP address unaweza kuiona ukigoogle what is my ip adress, tatizo la hii IP ni dynamic yaani inaweza kubadilika wakati wowote kutegemea na ISP wako anavyofanya kazi, ao itabidi umwelekeze mtumiaji aweke IP mpya kila wakati. Kama kweli una haja ya kurun server yako mwenyewe kuna ISPs wanaweza kukuuzia static IP ila gharama yake itazidi kutafuta server ya hosting.

Pia utahitaji kukonfigure router yako kuruhusu connection kutoka nje.
Angalia Making your local server accessible from anywhere | A web developer's blog
 
... zaidi ya hapo kama ISP wako anafanya NATing yaani watumiaji wengi wanatumia public IP moja basi hautaweza kufanya hiyo njia niliyotoa kwa kuwa public IP sio yako tu. Labda ungesema lengo lako ni nini haswa tungekupa mbadala.
 
... zaidi ya hapo kama ISP wako anafanya NATing yaani watumiaji wengi wanatumia public IP moja basi hautaweza kufanya hiyo njia niliyotoa kwa kuwa public IP sio yako tu. Labda ungesema lengo lako ni nini haswa tungekupa mbadala.
Lengo langu ni host website yangu pamoja na websites za wengine bila kutumia servers za wengine
 
Gharama ya kununua public static IP address inaweza ikarange kiasi gani? Na je hakuna ways ambavyo ukasubnet hiyo IP moja?
 
Gharama ya kununua public static IP address inaweza ikarange kiasi gani? Na je hakuna ways ambavyo ukasubnet hiyo IP moja?
 
Ukishapata hiyo IP unaweza kuwa na multiple sites hiyo ni configuration upande wa server.

Kwa bei hapa kusema ukweli sijui, ila fikiria vizuri, hii sio njia bora ya kuhost site. Umeme ukikatika itakuwaje? Hiyo machine yako ikiharibika au mtandao ukikata kwa sababu yoyote itakuaje?

Kama unajifunza mwenyewe basi fresh ila kama hizo site ni za wateja basi unajitafutia matatizo makubwa ni bora utafute shared hosting yenye multiple domains au reseller hosting, kama unataka kweli kukonfigure servers mwenyewe tafuta VPS kama digital ocean au OVH.
 
Mkuu mitandao ya 3G/4G huwa inablock incoming connections zote kutoka nje ya mtandao wao kwahiyo mtu outside Tigo kukupata kwa public IP yako inashindikana, lakini mtu anayetumia Tigo anaweza. Hili nilishawahi kulifanya kama jaribio.

Hata hivyo unaweza kutest kama computer yako inapatikana kwenye internet kwa kutumia huduma kama canyouseeme.org kwa kuingiza public IP yako (inakuwa autofilled pale) na port ya hiyo webserver/service yako (80 or ???)
 
So what is the solution?
 
Wacheki ttcl watakupa Public ip
 
broo unatakiwa kuwa na router then fanya kitu inaitwa port forwading
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…