Hicho king'amuzi cha ndani cha LG kinatafuta na kupata chaneli nyingi zinazotolewa na TING, STARTIMES, CONTINENTAL, DIGITEK. Ila nyingi zinakuwa zimefungiwa, zinaonekana lakini hazifunguki: kizungu wanasema zinakuwa "encrypted". Za Continental zilikuwa zinaonekana kabla hawajaanzisha utaratibu wa kulipia. Baada ya kuanza utaratibu wa kulipia, imebaki chaneli ya Star Religion, labda wamesahau kuifungia. Kwa sasa zinazoonekana ni za DIGITEK, kwa sababu wao hawajaanzisha utaratibu wa kulipia. Mimi kwangu nazipata zote za DIGITEK.