Chibidu
JF-Expert Member
- Dec 19, 2008
- 387
- 49
Wakuu poleni kwa majukumu mazito ya kuikwamua nchi yetu. Wakubwa naomba msaada wenu. Nimeitwa kwenye interview ya kazi kwenye kampuni moja ya usafirishaji. Tatizo langu ni kuwa, mara ya mwisho nilifanya interview wakati natafuta kazi mwaka 1998. Sasa nahisi nimepitwa na wakati, maana tangu nipate kazi mwaka huo sijawahi kuomba kazi nyingine mpaka leo na wala sijawahi kushiriki kwenye kuwafanyia watu interview. Wale wazoefu naomba mnisaidie, ni vitu gani siku hizi waajiri wanauliza sana? Nadhani mtakuwa mmenisaidia sana mimi na wengine wanaojiandaa kwa interview za kazi. Asanteni kwa kunivumilia